Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @chadematzofficial jimbo la Lupa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya kimezindua mikutano yake ya kampeni kwa ajili ya kuwanadi wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchagua viongozi kupitia CHADEMA.
CHADEMA kimeeleza kuwa viongozi wake ni waadilifu hivyo endapo watachaguliwa wataenda kusimamia haki, uwazi, uwajibikaji na utumishi shirikishi katika kuwatumikia wananchi.
Hayo yameelezwa na Katibu wa CHADEMA jimbo la Lupa, Yohana Mpamba (Mcotton), wakati akifungua mikutano ya kampeni katika kijiji cha Chokaa Chunya mjini ambayo itaendelea kufanyika ili wagombea wa chama hicho kunadi sera zao kwa wananchi.
Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mpamba (Mcotton amesema kuwa mji wa Chunya na wilaya ya Chunya kwa ujumla wake ni kongwe na ina utajiri mkubwa wa madini, ufugaji na shughuli za kilimo lakini bado wananchi wake ni fukara kutokana na miundombinu mibovu ya wananchi ikiwemo kurundikwa kwa michango inayotajwa kuwa ya maendeleo, kukosekana huduma muhimu kama maji na ukosefu wa huduma rafiki za kiafya pamoja na huduma mbovu za barabara.
Aidha, kiongozi huyo amewaomba wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni ya vyama mbalimbali ili kusikiliza sera za wagombea na kuwapima ili kwenda kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Wagombea wa nafasi mbalimbali kupitia CHADEMA walioshiriki ufunguzi wa kampeni hizo wamesema pamoja na hujuma za baadhi ya wagombea wenzao kuenguliwa lakini hawajakata tamaa na wana imani kuwa watashinda hivyo kuwaomba wananchi kuwachagua na kuahidi utumishi shirikishi kwa maendeleo zaidi tofauti na sasa wanapoona hamna maendeleo ya maana yaliyopatikana ndani ya miaka mitano iliyopita (2019-2024).