CHADEMA, CUF, ACT-Wazalendo, nk. jipangeni: Kuna nafasi ya kuwapiga CCM kwa ulevi wao

CHADEMA, CUF, ACT-Wazalendo, nk. jipangeni: Kuna nafasi ya kuwapiga CCM kwa ulevi wao

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,265
Reaction score
2,919
Nimeshaona jinsi CCM wanavyolewa maoni ya wanachama wao katika udiwani. Yaonekana hata katika Ubunge ulevi huo unaendelea. Baada ya 'wajumbe' kuwapitisha waliowaona kwa wema wao, wanaamini wapiga kura wote nchini pia watawapenda. Tulioko mitaani tunajua ni nini kinachozunguka vichwani mwa wananchi, nje ya vyama na wanachama.

Ushauri wangu kwa vyama vya Upinzani vyote ni kwamba umakini wenu ni mtaji. Pangeni yenu vizuri mkikumbuka kwamba wanachama wa vyama vya siasa ni wachache sana kuliko idadi ya wapiga kura. Mliowapitisha hakikisheni ni wale wanaokubalika kwa wapiga kura na siyo kwa chama chenu tu. Kwa mtindo huo, ulevi wa wana CCM utakuwa ni mtaji kwa upinzani.
 
Back
Top Bottom