29 November 2023
ZIFAHAMU SABABU KADHAA ZA CCM KUTEUA WAGOMBEA NGAZI ZA WENYEVITI WA MIKOA NA WILAYA BAADA YA KUFANGA UTENGUZI WALIOUITA WA KIUFUNDI
Picha toka maktaba: Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ikijadili hali ya kisiasa
Kanda ya ziwa habari ni kuwa uchaguzi utafanyika baada ya utenguzi wa kiufundi uliofanyika
Picha: Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu (katikati) akiwa na mkuu wa mkoa CPA Amos Makala (kushoto), wakati mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza,alipofika ofisi za CCM kujitambulisha.
Na kwamba uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, unakuja baada ya mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu kuteuliwa kuwa DED mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi. Ndugu Sixbert Jichagu alichaguliwa kwa kishindo kikubwa mwezi September 2022 lakini mwenyekiti wa taifa akampangia kituo cha kazi mwaka 2023 kuwa DED halmashauri ya Masasi.
Picha: mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo.
Wakati kwa mkoa wa Mbeya hamkani hali si shwari tena kisiasa kwa chama dola kongwe , mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo aliye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC alileta mtafaruku kwa kuhoji sababu za miradi mingi kusimama baada ya Magufuli kufariki.
Pia mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo alisema kunahitajika mjadala mpana kuhusu mkataba wa bandari na kuungana mkono wananchi walioomba kupatiwa sababu za, uhalali wa bandari kupewa DP World kwa mkataba ulioonekana kuwa na utata. Msimamo wa ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo ukaistua CCM na hata makamu wa rais akasema kuwa wanaCCM hawana utamaduni wa kuhoji waziwazi bila kupitia vikao vya ndani vya CCM kama alivyofanya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo mbele ya vyombo vya habari.