LGE2024 CHADEMA Dodoma mjini wadai kunasa majina feki ya wapiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Dodoma Mjini umelalamikia kuwepo kwa vitendo vya hujuma katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Daftari la Mkaazi.

Akizungumza leo, Oktoba 14, 2024, katika ofisi za CHADEMA Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilayani humo, Stephen Karashan, amedai kuwa wamebaini majina feki katika moja ya vituo vya uandikishaji wa wapiga kura.

Soma Pia:
Karashan ameongeza kuwa vitendo hivi vinahatarisha uadilifu wa mchakato wa uchaguzi na kuitaka serikali kuingilia kati kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa haki na uwazi.

Your browser is not able to display this video.
 
Kila mwaka mnalalamika na bado mnashiriki.
 
4R za mchongo.......wizi mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…