CHADEMA fanyeni haya kumng'oa huyu mkoloni mweusi

CHADEMA fanyeni haya kumng'oa huyu mkoloni mweusi

Mtemi Mbojo

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
891
Reaction score
1,569
Nikiwa kama mpenda demokrasia ya kweli na mtu niliyefadhaishwa na namna chaguzi zetu zinavyoendeshwa. Ningependa kuchangia yafuatayo kwa chama cha CHADEMA, chama hiki angalau kinabeba matumaini kwa wapenda demokrasia ya kweli

1. Chama kianzishe RUNINGA na RADIO yake, ndani or hata nje ya nchi hasa hizi nchi jirani kama Kenya kwa ajili ya kuibua ufisadi, changamoto na kutoa njia mbadala ya kutatua changamoto hizo bila kusahau kueneza SERA na ITIKADI za Chama

2. Ipigwe movement ya nguvu ya KUDAI KATIBA MPYA NA ILIYO BORA pamoja na TUME HURU NA SHIRIKISHI YA UCHAGUZI. Chama kipeleke vijana kujifunza mbinu zaidi ya kufanikisha haya. Kuna mengi ya kujifunza nchi jirani ya Msumbiji na hata Kenya hasa kipindi cha Hayati MOI. Pia ni vyema mkahusisha makundi mbalimbali kama vyama ya kiharakati,viongozi wa dini, diaspora, vyama vya kitaaluma

3. Iendeshwe kampeni kali nje ya nchi hasa haya Mataifa yanayotufadhili bajeji zetu za Maendeleo,i li waelewe kwamba hakuna demokrasia ya kweli nchi. Kusanyani EVIDENCES za KUTOSHA na kuziwasilisha kwa wafadhili. Njia hii aliitumia sana Hayati Maalim seif na Mh Lissu kuonyesha duna ufedhuli wa Serikali hii ya CCM

4. Elimu ya Uraia izidi kutolewa hasa vijijini. Uzuri sasa vijana wengi hata vijijini wana Elimu ya Kidato cha nne,naamini wanaellimika kirahisi

5. Kuwe na mikakakti ya kutafuta vyanzo endelevu vya FEDHA,na hizi kanda ziongezewe nguvu

6. Mikutano ya hadhara ya kutosha bila kusahau maandamano ya kupingika mambo yote yasiyofaaa

N.B
Kuiondoa CCM sio kazi rahisi, kwa kuwa wanajua siku wakitolewa madarakani basi wengi wao watafikishwa Mahakamani kwa UFISADi
 
Nikiwa kama mpenda demokrasia ya kweli na mtu niliyefadhaishwa na namna chaguzi zetu zinavyoendeshwa.Ningependa kuchangia yafuatayo kwa chama cha CHADEMA ,chama hiki angalau kinabeba matumaini kwa wapenda demokrasia ya kweli

1. Chama kianzishe RUNINGA na RADIO yake, ndani or hata nje ya nchi hasa hizi nchi jirani kama Kenya kwa ajili ya kuibua ufisadi ,changamoto na kutoa njia mbadala ya kutatua changamoto hizo bila kusahau kueneza SERA na ITIKADI za Chama

2. Ipigwe movement ya nguvu ya KUDAI KATIBA MPYA NA ILIYO BORA pamoja na TUME HURU NA SHIRIKISHI YA UCHAGUZI .Chama kipeleke vijana kujifunza mbinu zaidi ya kufanikisha haya. Kuna mengi ya kujifunza nchi jirani ya Msumbiji na hata Kenya hasa kipindi cha Hayati MOI. Pia ni vyema mkahusisha makundi mbalimbali kama vyama ya kiharakati,viongozi wa dini, diaspora ,vyama vya kitaaluma

3.Iendeshwe kampeni kali nje ya nchi hasa haya Mataifa yanayotufadhili bajeji zetu za Maendeleo,i li waelewe kwamba hakuna demokrasia ya kweli nchi. Kusanyani EVIDENCES za KUTOSHA na kuziwasilisha kwa wafadhili. Njia hii aliitumia sana Hayati Maalim seif na Mh Lissu kuonyesha duna ufedhuli wa Serikali hii ya CCM

4.Elimu ya Uraia izidi kutolewa hasa vijijini. Uzuri sasa vijana wengi hata vijijini wana Elimu ya Kidato cha nne,naamini wanaellimika kirahisi

5.Kuwe na mikakakti ya kutafuta vyanzo endelevu vya FEDHA,na hizi kanda ziongezewe nguvu

6. Mikutano ya hadhara ya kutosha bila kusahau maandamano ya kupingika mambo yote yasiyofaaa

N.B
Kuiondoa CCM sio kazi rahisi,kwa kuwa wanajua siku wakitolewa madarakani basi wengi wao watafikishwa Mahakamani kwa UFISADi
Ongeza hii: Kuwa na strong tawi la chadea Diaspora ambao watasema na kutoa mikakati yote ambayo wataona inafaa kuwaondoa ccm madarakani. Wao wako nje watakuwa safe kusema/kufanya yote wanayoyafikirini mema kwa nchi yetu bila polisi/TISS kwateka.

Otherwise umeandika vizuri kabisa
AIONE Erythrocyte
 
Pia itengenezwe documentary inayoeleza mauaji yote ya wanachama wa wapinzani yaliyofanywa na CCM na vyombo vyake tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi kisha isambazwe kwa vyombo vyote vikubwa vya habari duniani kuelezea unyama wa serikali ya CCM.Lazima sasa kupambana na CCM kwa mbinu zote.
 
Media itafanyiwa figisu na hatimaye kufa kabisa. Unalikumbuka gazeti la MAWIO?

Iacheni ccm ibakie peke yake, tuwe na chama kimoja. Au unaonaje mleta mada?
 
Back
Top Bottom