Zanzibar 2020 CHADEMA: Hadi sasa watu watatu wamejitokeza kutaka Urais wa Zanzibar akiwemo Mohammed Ayoub

Zanzibar 2020 CHADEMA: Hadi sasa watu watatu wamejitokeza kutaka Urais wa Zanzibar akiwemo Mohammed Ayoub

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
403C29D7-607B-4DE7-BA1D-4E822BD4BD6E.jpeg

Mohamed Ayoub

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuwataarifu umma wa Watanzania kupitia Mkutano huu kuwa jumla ya Wanachama 3, wamejitokeza kutia nia kuwania uteuzi wa kupeperusha bendera, kugombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu, ambao utahusisha pia nafasi za Udiwani, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Ubunge.

Wanachama hao ambao idadi yao itatangazwa rasmi kwa umma kupitia taarifa hii, kwa vyombo vya habari, wamejitokeza ndani ya muda uliowekwa kutangaza nia hiyo kwa kutekeleza kifungu cha (1) cha Mwongozo wa Chama wa kutangaza kusudio la kuwania Nafasi za Uongozi kwenye Vyombo vya Uwakilishi Serikalini, kipengele cha (g), ambacho kinataamka;

“Kwa Nafasi ya Uongozi wa Kitaifa ndani ya Chama na Urais taarifa za walio na kusudio la kugombea nafasi hizo zitawasilishwa kwa Katibu Mkuu na kujadiliwa na Kamati Kuu na kutolewa uamuzi kwa taarifa zinazofuata.”
Mtakumbukwa mnamo Juni 06, mwa huu,

Ofisi kuu ya CHADEMA Zanzibar kupitia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe Salum Mwalimu alifungua rasmi milango kwa mwanachama yoyote anaye taka kutia nia nafasi ya Urais, kuandika barua ya kusudio lake kwa Katibu Mkuu.

Hadi mlango huo wa kutia nia unafungwa Juni 15, mwaka huu, saa 10.00 jioni, wanachama waliotekeleza kanuni hiyo ni hawa wafuatao;

Hashim Juma Issa
Mohamed Ayoub Haji
Said Issa Mohamed

Aidha mwanachama mmoja ametia nia kwa njia ya simu. Hata hivyo kwa kuwa bado hajakamilisha baadhi ya taratibu kwa sasa hatutataja jina lake.

Chama kitatoa utaratibu utakao fuata baada ya kukamilisha taratibu za ndani ya Chama. Kwasasa watia nia wote hawa wanapaswa kuendelea kuzingatia taratibu za chama mda wote.

Hata hivyo, Chama kinawakubusha wanachama wake kuwa kushindwa kutangaza nia hakumnyimi mwanachama kushiriki mchakato huu katika hatua za uchukuaji fomu.
 
Huko Zanzibar, CHADEMA wawaunge mkono ACT, na ACT nao wawaunge mkono CHADEMA huku bara, ila tatizo kubwa linabaki ni kutokuwepo kwa tume huru.
wapi chadema mlishindwa kuitumia CUF vizuri Duni Haji mkamtoa kama mbwa akatimukia ACT wazalendo. Uhuni wenu chadema sasa ndio unatiwa nukta mlijifanya wajanja mtakula jeuri yenu.Matapeli WA kisiasa nyie
 
wapi chadema mlishindwa kuitumia CUF vizuri Duni Haji mkamtoa kama mbwa akatimukia ACT wazalendo. Uhuni wenu chadema sasa ndio unatiwa nukta mlijifanya wajanja mtakula jeuri yenu.Matapeli WA Julissa nyie
hujui kitu !
 
Ugombea uraisi chadema Safari hauna mvuto kabisa chadema kwisha
 
Chadema leo wametoa fomu kwa wanachama wake wanaotaka kugombea urais wa Zanzibar.

Wanachama watatu wamejitokeza na kukabidhiwa fomu na mkurugenzi wa uchaguzi wa Chadema kanda ya Zanzibar mh Salim.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Ugombea uraisi chadema Safari hauna mvuto kabisa chadema kwisha
Kinyume chake ndio unachotaka kusema manake dikteta wenu kashakataa mtu asishindane naye unafikiri mvuto haupo CDM au ccm.
 
Back
Top Bottom