Acid
Hivyo vibendera kwenye vibanda na maduka visikutishe. Hata mimi kwenye genge ninalomiliki ipo bendera ya CCM. Wala haihusiani na mapenzi kwa chama hicho. Ila CCM wanapandikiza hofu fulani kwamba ukiweka hiyo bendera, wewe uko kwenye safe side.
NB: Ni wananchi wenye nguvu na uwezo wa kuchagua chama wanachokitaka.
Nadhani CHADEMA wanahitaji kuwa open minded na kutafuta mkakati makusudi ambao utawafanya wawafikie watu kwa ukaribu na sio kupitia kwenye majukwaa tu. Hio ndio inawafanya watu wawe karibu na kukiamini chama.Chadema na chama chengine cha siasa kitapata tabu kubwa kushinda hadi kitakapogeuka kuwa household name.
Yaani katika kila mazungumzo hata yasiyohusiana na siasa kiwe kinatajwa.
Tunahitaji kupenyeza idea za chama kwenye levels zote za kijamii ili hata Yule asiyekuwa na nafasi ya kusikiliza siasa akienda kupiga kura chama cha karibu kwake kisiwe ccm
Nadhani invincible amesahau ile hadithi kauli ya 70% ni bendera!!!Mazee unaweza kutengeneza perception ya kwamba CCM ina support kubwa kuliko ilivyo, na wengine wakapiga kura kwa kufuata perception hii.
Kuna watu kibao wanapiga kura kwa kuangalia nani yuko popular, na bendera nyingi ni zipi, sad as it may sound.
View attachment 12675View attachment 12677View attachment 12676Nikilinganisha kwa muonekano wa picha za mikutano kati ya CCM na CHADEMA naona kuna kundi kubwa la wapiga kura nalikosa kwenye picha za CHADEMA, si waongeaji sana lakini ndio huamua nani awe kiongozi kutokana na nguvu yao ya kujitoa, uvumilivu na uwingi wao. Kwa waliofika kwenye mikutano labda kamera huwa haziwaoni, Je wapo wapiga kura hawa?
Kwanza hizo picha umezi-crop! Pili, ile ya katikati si rahisi kujua jinsia wala umri kwa jinsi ilivyo ndogo, mwishio mimi sipo kwenye hizo picha lakini mwaka huu nitapiga kura - nampa Dr. Slaa!!!!!!!!