Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Zaidi ya mara moja kiongozi wake muandamizi ambae pia ni makamu mwenyekiti wa Taifa wa chama hiki amebainisha wazi na kulalamikia jambo hili baya kabisa, linalokwamisha mambo mengi sana kusonga mbele ndani ya Chadema na mahali pengine popote. Rushwa.
Alilizungumzia jambo hili la rushwa nje ya utaratibu wa vikao vya ndani vya chama chake kwa uchungu sana kudhihirisha na kuthibisha kwamba ndani ya uongozi wa chama hicho hakuna meno ya kung'ata mfupa huu mgumu sana, na wala hakuna kitu kinaweza kufanyika kuwashughulikia wahusika rushwa hiyo ndani ya chadema.
Ni kama vile rushwa ni mtindo wa maisha ndani ya chama hicho kikongwe cha siasa na imeshindikana na ina malezi chini ya uongozi uliopo.
Kwa maelezo yale ya makamu mwenyekiti, ni dhahiri hakuna hatua ambazo Chadema imechukua au inaweza kuchukua dhidi ya wala rushwa tena uongozini.
Wala hakuna nia, dhamira au mipango mikakati madhubuti ya kukabiliana na ufisadi wa aina yoyote ndani ya chama hicho muhimu kama vilivyo vingine katika siasa za Tanzania.
Kuna kila dalili kwamba wala rushwa ndani ya chama hicho wana nguvu mno, kiasi cha kumtisha kiongozi huyo muandamizi mwenye uwezo wa kuchukua hatua kabisa, lakini anajawa hofu na kuamua kukimbilia kuwashitaki kwa wanachama kwenye majukwaa ya kisiasa na kwa wananchi.
Kama wameshindwa kukabiliana na rushwa ndani ya chama chako, wanaweza kweli kukabiliana na uhalifu waliotuja leo nje ya chama?
Hii si hadaa ya kuteka hisia za wananchi na kutafuta huruma kwa waTanzania licha ya kwamba tuhuma wanazoibua ambazo si mpya zinashughulikiwa na mamlaka husika za kiuchunguzi ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Ni muhimu sana kama Taifa, kua wastahimilivu na wenye subra, kusubiri matokeo ya kiuchunguzi yanayoendelea.
Hakuna haja ya kuchochea na kuwajengea watu hofu na chuki dhidi ya vyombo vya kiuchunguzi vya ulinzi na usalama nchini.
Tuwape nafasi, tuwape muda wafanye kazi yao vizuri kwa haki , uhuru, usawa na usahihi ili haki itendeke kwa kila mTanzania 🐒
Mungu Ibariki Tanzania