Uchaguzi 2020 CHADEMA hawakuwaandaa Wagombea wake katika kuelewa sheria, kanuni na muongozo wa Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 CHADEMA hawakuwaandaa Wagombea wake katika kuelewa sheria, kanuni na muongozo wa Uchaguzi Mkuu

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2018
Posts
439
Reaction score
742
CHADEMA isitafute mchawi kuenguliwa kwa wagombea wake katika nafasi za Udiwani na ubunge kwenye uchaguzi mkuu ambao kampeni zake zimeanza tangu Agosti 26, 2020 kwani hawakuwaandaa wagombea wake katika kuelewa sheria, kanuni na muongozo wa uchaguzi mkuu chini ya NEC.

Walishindwa kutoa wanasheria kama wanavyosimamia kesi za viongozi kuzunguka kanda kwa kanda kuhakikisha wagombea wote wanajaza fomu kwa usahihi na kukidhi taratibu zinazotakiwa?

Mfano: Mgombea ubunge jimbo la Moshi Vijijini Lucy Owenya kama anavyofahamika alijaza jina tofauti na vitambulisho vyake vya Taifa badala yake anajaza majina ya a.k.a, Kura na Leseni yake ya gari. Pia alishindwa kujaza jina la chama chake kinachomdhamini pamoja na kutokusaini fomu ya uteuzi. Sasa makosa ya aina hii unamlaumu nani?

Picha hizi hapa chini zitakusaidia uelewa.

IMG-20200828-WA0046.jpg
IMG-20200828-WA0045.jpg
IMG-20200828-WA0050.jpg
IMG-20200828-WA0046.jpg
IMG-20200826-WA0011.jpg
IMG-20200826-WA0011.jpg
 
Kuna yule wa Mtama aliyenyang'anywa form na TAKUKURU mezani kwa mkurugenzi wakati anazirejesha na huyu naye hakuandaliwa kuwakwepa maofisa wa TAKUKURU? CCM kushirikiana na Tume,Polisi, TAKUKURU na wahuni wengine wamevuruga mchakato mzima huu. Tumeshiriki uchaguzi chini ya mfumo wa vyama vingi tangu 1995 lakini hatujawahi kushuhudia uharamia huu. Ni dhahiri utawala wa awamu hii ndiyo umeasisi uharamia huu.
Na inasikitisha kuona watu hasa viongozi wa dini wanashindwa kukemea ushenzi huu na badala yake lawama wanashushiwa wahanga wa uonevu. Lakini kama Mungu aishivyo muasisi wa uharamia huu mwisho wake utakuwa wa mateso makubwa. Haiwezikani mtu aligawe Taifa kwa chuki za kiitikadi za kisiasa,kidini, kikabila na kikanda akabaki salama. Mungu yupo na hajalala usingizi.
 
Akienguliwa dawa wanasema ni kuandamana nyuma ya keyboard.
 
CHADEMA isitafute mchawi kuenguliwa kwa wagombea wake katika nafasi za udiwani na ubunge kwenye uchaguzi mkuu ambao kampeni zake zimeanza tangu Agosti 26, 2020 kwani hawakuwaandaa wagombea wake katika kuelewa sheria, kanuni na muongozo wa uchaguzi mkuu chini ya NEC.

Walishindwa kutoa wanasheria kama wanavyosimamia kesi za viongozi kuzunguka kanda kwa kanda kuhakikisha wagombea wote wanajaza fomu kwa usahihi na kukidhi taratibu zinazotakiwa?

Mfano: Mgombea ubunge jimbo la Moshi Vijijini Lucy Owenya kama anavyofahamika alijaza jina tofauti na vitambulisho vyake vya Taifa badala yake anajaza majina ya a.k.a, Kura na Leseni yake ya gari. Pia alishindwa kujaza jina la chama chake kinachomdhamini pamoja na kutokusaini fomu ya uteuzi. Sasa makosa ya aina hii unamlaumu nani?

Picha hizi hapa chini zitakusaidia uelewa.

Huu ushenzi wako hauna nafasi hapa.
 
Back
Top Bottom