Uchaguzi 2020 CHADEMA hawatafurukuta 2020

Uchaguzi 2020 CHADEMA hawatafurukuta 2020

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
3,216
Reaction score
990
Baada ya kutoka na Tundu Lissu kama mgombea Urais kwa upande wa CHADEMA hiyo ilikuwa sahihi na jambo tulilolitegemea.

Kuhusu mgombea mwenza Salum Mwalim hapo nawapa pole huyo jamaa aliwaponza 2015 na kupoteza majimbo kadhaa kwa uzembe wake wa kutokuheshimu wagombea wanaokubalika.

Upande wa Zanzibar ndiyo wamelamba galasa kabisa wataambulia patupu. Kwanini hawakutumia mwanya wa nipe nikupe?

Naamini Membe asingekataa kumwachia Tundu Lissu kama wangekuja na turufu ya kumwachia Maalim Sefu Zanzibar kupitia ACT. Na ukiwasikiliza utaona hawaoni sababu ya kuachiana na vyama vingine vya upinzani.

Wana mtizamo utakaokuja kuwashangaza mwisho watakapoanguka vibaya. Lakini tunaona kabisa hata leo kuwa matokeo yao yatakuwa mabaya sana mwaka huu 2020.
 
CCM mmemwaga bilioni mbili kwa wajumbe Tundu Lissu asipite, apite Nyalandu, hela yenu inapigwa mande pale 5N na wajumbe, nendeni mkajioneee jinsi mlivyopigwa changamoto la macho
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom