Nyerere hakupindua TAA. Walioleta mabadiliko TAA ni wakina Sykes, Mwapachu, Dr. Kyaruzi na wengine walipowaondoa katika uongozi wazee wao Thomas Plantan na Clement Mtamila mwaka 1949. Hawa waliongoza TAA ( Dr. Kyaruzi halafu Abdulwahid Sykes) mpaka 1953 ambapo Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wake. Nyerere na wenzake walibadilisha jina la TAA kuwa TANU mwaka 1954. Unataka kutuambia Nyerere alijipindua mwenyewe kama Rais wa TAA?
Amandla...