CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Hata mimi ni hivohivo ndugu yangu.
Kiukweli kabisa CHADEMA iliusaliti UMMA wa watanzania 2015.
...Haijatubu, haijajifunza na siioni CHADEMA ile ya NGUVU YA UMMA ikirudi kwa sababu watu wote wenye akili waliishtukia.
 
Kwa mtazamo wangu, Mabere N Marando na Marehemu Augustino L. Mrema hawakuwa wanamageuzi sahihi.

Yalikuwa ni mapandikizi ya mashushushu mahususi yaliyomwagwa upinzani.

Mrema alipojiunga na Nccr na kugombea Urais, kila mpenda mageuzi alimuunga mkono na kama siyo figisu za Ccm, '95 angelichukua nchi.

Lakini baada ya hapo ndiyo nikagundua kuwa kumbe lilikuwa ni zimwi halisi la kuhujumu mageuzi!

Hama hama sana vyama, na kila alipohamia lazima akapavuruge, hadi alipokuja kutuama Tlp na kukiunga mkono Ccm waziwazi karibia na siku zake za umauti.
 
Na mwisho wa siku nani kaibuka mshindi? Chadema ipo Magufuli alikufa kibudu.
 
Duh, yaani umepatia vema wasifu wa huyu mtu.
 
Hahahaha mkuu hakuna kitu naheshimu kama MKE WA MTU labda sijui itokee dharura gani huko ama bahati gani mbaya..Lakini kwa hali ya kawaida kabisa kwangu hiyo ni haramu
Nimecheka sana hapo 'labda sijui itokee dharura gani huko au bahati mbaya gani....'
 
Anaweza akawa ni mmoja Kati ya watu waliotapeliwa na kijana wa mbowe
 
Na huu ndiyo ukweli wenyewe
 
Sasa sijui leo umeandika kitu gani hiki mkuu Mshana jr. Ulosi wote ule unaosifiwa nao, na umakini mwingi uliojidhihirisha nao katika jukwaa hili bado unafumbafumba mambo kama kigori asiyewahi kuonja?

Mimi nitakisia/bahatisha huyo unayemzungumzia hapa kuwa ni mtu anayejiita Paskali, ambaye mimi sitambui kamwe kuwa anao unguli wowote wa kiuandishi unaoo usema wewe hapa. Mtu anayejaza matakataka katika mtandao mzima wa JF, leo hii unampamba kuwa mwandishi nguli?
Paskali 'Njaa' anao uandishi upi wa kuifanya CHADEMA itetereke? Ilaumu CHADEMA yenyewe kushindwa kukoga nyoyo za waTanzania kwa uzembe wao wenyewe na wala siyo kwa uandishi wa kikanjanja unaofanywa na huyo unayemlalamikia humu.

Habari za huyo Bagenda na Mzee wa kilalacha sizijui, na wala sidhani kuwa ni mfano sahihi wa ulinganisho hapa. Ninachojuwa ni kuwa Mzee alijiishia nguvu mwenyewe na kupoteza mwelekeo hadi hapo umauti ulipomkuta.
 
Niliacha kusoma magazeti yake na kidhungu cha naniluuu... Maandishi yake yanachosha yanalegesha yanaudhi yana ukakasi
Mungu tujalie uzee mwema
Huyu asituchoshe

Kwema huko rafiki!!
Kusema kweli leo nimemshangaa Mshana kupoteza muda wake kuleta mada kama hii hapa Jukwaani!
Sijui ni makala gani ya huyo mtu iliyomuumiza moyo kiasi cha kuamua kuiandikia mada humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…