CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Hivi Mzee Bagenda amefariki mwaka gani? Nisaidie...tafadhali!🙏🙏🙏
 
Pamoja na mapungufu mengi kwa mitazamo ya walio wengi ya Pasco mayala lakini ukweli chadema ni kama sio tena sauti ya wengi, sio mkombozi tena kama tulivyodhania wakati ule, tunaweza kuandika mengi lakini chadema kimekua na mapungufu mengi sana nyakati hizi tokea 2015 kuja huku tulipo.

Niko na kadi ya chadema tokea 2004 na nimepiga kura kwa mbowe, slaa,. Lakini ile 2015 kwa kweli hapana, walao 2020 lakini nako walikuwa hawako serious.

Na kwa mwendo huu miaka kumi ijayo tutakuwa tukiona chadema kama tlp au caf kama sio udp kabisa.
 
Wengi wanaokaribia kufa kwa mipango ya Mungu huwa wanafanywa daraja la Uharifu na ufitini kwa kulipwa
 
Ifikie hatua akili zetu zikue na zikomae kuendana na falsafa ya kile kinachopiganiwa....... Demokrasia ni pamoja na kuvumiliana, kuheshimiana kwani tupo kwenye ulimwengu ambao kila mtu ana maoni yake..........

Usitarajie kuyakuta tu yanayokufurahisha tu.....

Mtiririko wa mada zinazozungumzia mtu ambaye ametofautiana na watu maoni ni dhahiri kuwa tuna safari ndefu kuelekea kwenye demokrasia....
 
 
Hapo ulipoandika hakuna aliewahi kupambana na asiejibu akashinda panafikirisha

Maana wafuasi wa Chadema mnaongoza kumtukana Magufuli huku mkijua hawezi kujibu kwasasa

All in all mengne watajibu wengine lakini la muhimu tukosoane kwa hoja sio vihoja.
 
Niliacha kusoma magazeti yake na kidhungu cha naniluuu... Maandishi yake yanachosha yanalegesha yanaudhi yana ukakasi
Mungu tujalie uzee mwema
Huyu asituchoshe

Kwema huko rafiki!!
Nimekuhamu rafiki mwema.. Mbona umekuwa adimu siku mbili tatu hizi? Hope all is well
 
Maana wafuasi wa Chadema mnaongoza kumtukana Magufuli huku mkijua hawezi kujibu kwasasa
[emoji15][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827] Nadhani hizi ni tuhuma mpya zisizo na ithibati
 
BAVICHA katika kuendeleza udikteta. Wanachokisema wao wanaita “sauti ya umma”, wamejipachika cheo!
Mtu akiwa na maoni tofauti na wanavyopenda kusikia atakumbana na matusi na propaganda za kulazimisha kumchafua! Anayesemwa kwenye threads zake anawazidi hoja kwa mbal, ukisoma hoja za BAVICHA ni matusi tu na ujinga Mwingi.
Sasa wanatumia mbinu ya kuandaa threads za kumtisha na lawama lukuki. Alafu wanajiita chama cha demokrasia!
 
Maana wafuasi wa Chadema mnaongoza kumtukana Magufuli huku mkijua hawezi kujibu kwasasa
[emoji15][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827] Nadhani hizi ni tuhuma mpya zisizo na ithibati
Hoja yangu hiyo nimeijenga kwa kuangalia wafuasi wa mitandaoni haswaa humu jamii forums

Karibu kila siku lazima atatukanwa kwa neno la namna yoyote lile

Naiman hata nafsi yako inaujua huo ukwel ila tu unazuga kama ni jambo jipya

Siku nilipoona uzi wa Zitto akikosolewa kumuita kiongozi mwenzie Chiba nilisema wazi Zitto kakosea

Ila pia nikaweka angalizo kuwa tusipende kuwakashifu wengine ili wapendwa wetu wasikosolewe pia

Humu kuna wajinga wamewahi kumdhihaki Mbowe,Zitto,Magufuli,Lissu,Ndugai,Tulia n.k

Ila kwavile tunajali sana itikadi kuliko ubinadamu kila upande unaona sawa

Najua Magufuli kuna mambo alikosea kama binadamu na kuna aliyopatia pia kama binadamu kuendelea kumtukana haijengi lolote zaid ya kupoteza muda

Tupambaneni kuondoa huu ugumu wa maisha kwa jamii yetu kwa kuwashauri njia nzuri viongozi wetu.
 
Sahihisho,mzee Prince Bagenda bado yuko mzima kabisa,japo umri umekwenda lakini yuko mzima kabisa na hata mchana wa leo niliwasiliana nae. Hata ukihitaji kumsalimia nitafute nikupatie namba umsalimie.
Ule msukosuko wakati wa jiwe ulikwisha.
 
Jibuni hoja na sio kuyafanya mambo too personal, yuko na haki ya kueleza fikra zake, hamumjibu na hapa unafanya nini? eti "wengi", kila siku tunawaambia ingieni mtaani ili muwaine hao wengi ni akina nani...angekuwa anaongea uongo basi ungekuwa na hoja, kwa nini hamtaki watu wajue kwamba katiba yenu inazuia wanachama kwenda mahakamani kinyume na katiba ya nchi? kwa nini hampendi watu wajue ukweli kwamba taratibu zilikiukwa katika kuwaadhibu wabunge wenu? katiba yenu tu inawashinda ya nchi mtaweza kuilinda kweli?
 
Sahihisho,mzee Prince Bagenda bado yuko mzima kabisa,japo umri umekwenda lakini yuko mzima kabisa na hata mchana wa leo niliwasiliana nae. Hata ukihitaji kumsalimia nitafute nikupatie namba umsalimie.
Ule msukosuko wakati wa jiwe ulikwisha.
Asante sana kwa mrejesho huu naenda kufuta kauli

Ila ningetamani atuambie ile project ya kumchafua Mrema ilikuwa na lengo gani.. Ukiweza muulize tafadhali
 
Asante kwa kuleta Kiki hapa kwa ujumla huyu mwandishi anayejiita Nguli. Pascali njaaa ni kisirani na ndio maana ameendelea kuupiga.
Kwani CDM walikukosa nini?!

Sent from my SM-A115AZ using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…