CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Hata kama Covid 19 wakibebwa hadi 2025 Chadema haina cha kupoteza mbele ya jamii, imeonyesha inasimamia inachokiamini iko consistent, serikali ndio itakayojidhalilika kupitia vyombo vyake vya Bunge, NEC, ofisi ya Msajili na mahakama.
 
Hapo tu ndio huwa Chadema wanapokosea.

Huwezi ukalazimisha watu wafikiri namna mnavyofikiri.

Kila mtu ana utashi wake.

Katika maisha ni vyema tukaheshimu mitazamo ya wengine.

Kuanza kumjadili mtu badala ya issues ni dalili ya kuishiwa.
 
Kama anakisema vibaya CHADEMA, basi ninyi kisemeni kwa mazuri Watanzania tutaelewa tu.
 
Asante kwa kumuonya. However, I guess it is too late now. Mie nimeshawasilisha kesi rasmi mahakama ya mwisho. Nimeweka maandiko yake 2 ya kuishtumu CDM ambayo nimeomba mahakama iyapitie na kuona Kama ni ya haki ama la.Nimeomba mahakama baada ya kupitia nyaraka hizo itoe hukumu dhidi ya upande usio na haki kwa kadri inavyoona inafaa.
NB. Wakati wa magufuli pamoja magufuli kuwa na kesi nyingi sana nilichagua kuwasilisha mbele ya mahakama kesi moja tu ya Akwilina. Mahakama ilikubali maombi yangu siku ile Ile na nikapewa miezi 6 ya hukumu kutekelezwa. Miezi SITA haikufika.
 
Yeah kuna mdau huko nyuma keshasema hivyo [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mahakama ilikubali maombi yangu siku ile Ile na nikapewa miezi 6 ya hukumu kutekelezwa. Miezi SITA haikufika..[emoji31][emoji848][emoji2827]
 
Mienendo ya mwenyekiti wa CHADEMA inatia mashaka zaidi katika kuhujumu chama kuliko huyo mwandishi. Think beyond your conditioned limits.
 
Upotoshaji au usahihi wa jambo ni tafsiri ya kimapokeo au matokeo ya kimapokeo.....pamoja na yote kama usahihi unafahamika na wengi na yeye anapaswa kufahamishwa kama atasimamia kile anachokiamini anapaswa kuachwa na utashi wake na sio kutukanana na kudhalilishwa....... Demokrasia sio tu kuitamka bali na kuiishi....na kuiishi ni pamoja na kuvumiliana
 
Sasa ikiwa wew ni Chadema kindakindaki unashangaa nini huyo mwandishi kuiponda chadema maana yake na yeye ana Imani yake
Mimi nadani tusidhani demokrasia ni kutendeka unachokitaka wew na ikiwa kinyume unaona nongwa
Umeambiwa abalance story aandike uhalisia kama CHADEMA wamekosea aseme na kama Tulia amekosea aseme.
 
Tuwe kwakweli bila kupelekwa na mahaba kiitikadi.Pascal kakosea nn !? Yeye kaeleza kile ambacho anaona kilipaswa kufanywa kwa jinsi ya utaratibu kwa uzoefu wake

Tungejib hoja zake na sio kuaattack personality yake
 
Ukiangalia kwa makini sana mwandishi huyo unayemtuhumu ana kishambulia Chadema, Tena ukitumia jicho la Tatu(najua una macho zaidi ya Matatu), utagundua mwandishi huyu ana nia njema na Chadema wakati huo huo anaitakia mema Tanzania.

Kile unachokiita kukishambulia Chadema kutoka kwa mwandishi huyu ni jitihada zake za kuhakikisha Chadema kinajisafisha, kuimarika, kwa kufuata taratibu zake kilichojiwekea, ili kidhibitishe kuwa kitafuata sheria za nchi na katiba ya nchi pindi kitakapofikia hatuna ya kukabidhiwa madaraka.

Mwandishi ana nia njema na Tanzania, ndiyo maana anaona chama chenye mwelekeo kuwa mbadala wa CCM hapo baadaye (baadaye haifiki kama hatuna chama imara mbadala), ni Chadema. Anataka Tanzania ikabidhiwe kwa Chama cha Kitaifa na chenye mlengo wa kuwaunganisha watanzania badala ya kuwatenganisha kwa Kanda.

Kwa hiyo, mwandishi anaking'arisha Chadema. Tumia vizuri jicho la Tatu utagundua hilo.
 
Kwa vile Chadema ni Chama cha Mungu , shetani hujidhihirisha mwenyewe
Dah, kamanda nenda katubu na ufunge kabisa kwa wiki nzima kupata radhi ya M/Mungu.

Kusema cdm ni chama cha Mungu ni sawasawa na kusema Mungu anapenda wivu, upendeleo, uongo, hila, chuki, ubaguzi, matusi na utengano. Hili si sawa labda km kuna 'mungu' mwingine unamzungumzia tofauti na huyu tunayemuabudu.

Ushauri; tuepuke kumtumia Mungu km fursa au daraja katika kutafuta kuungwa mkono katika usheitwani wetu,...........hasira zake ni kali sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…