CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Mimi sina tatizo na Paskali kuiandika CDM vibaya maana ndio uhuru wa maoni. Na huenda kwenye kuisema vibaya huko baadhi ya mapungufu ya CDM yanaweza kurekebishwa. Ila ni kwanini Paskali anaisema vibaya CDM, hapo ndio kwenye mjadala.
  1. Paskali anaisema CDM kwakuwa ana wivu nayo kutokana na kuwa yeye ni mwanaccm, na CDM ina ushawishi mkubwa kwa umma bila kutumia vyombo vya dola. Inshort ana nongwa kubwa na CDM, hata akitoa ushauri sio wa nia njema, bali ni wa kinafiki zaidi.
  2. Paskali anapenda kutumia mitandao, na huku kwenye mitandao CCM haitambi kama ilivyo CDM, kwani huku mitandaoni hakuna vyombo vya dola vya kuibeba CCM na kuikomoa CDM. Hivyo Paskali anakutana na mashambulizi yanayomkera toka kwa wafuasi wa CDM, sasa anaandika kila mara kuhusu CDM maana anajua post yake itapata replies nyingi hata kama ni negative kwake, na ni sehemu ya kurelease stress zake kutokana na kejeli anazopewa na wafuasi wa CDM.
  3. Hili nadhani ni sehemu ya haya mabandiko yake ya sasa. Toka wakati wa Magufuli kuna mpango wa kuanzisha chama kingine ili kuchukua nafasi ya CDM, ndio hiki umoja party. Na namna pekee ilikuwa ni lazima CDM ife kwanza kisha kiingie chama kingine. CCM wanajua fika wameshapoteza mvuto, ila hawako tayari kuwaachia Cdm wachukue nchi kwa ajili ya usalama wa viongozi wake, hii ni kutokana na uhuni na wizi walioufanya. Sasa system wakatengeneza mpango wa kuanzisha chama kingine, lakini lazima CDM ife kwanza, kwani ndio yenye wafuasi wengi wa kweli kuliko ilivyo vyama vingine. Namna ya kuiua CDM ni pamoja na kutengeneza migogoro ndani ya CDM, kununua wanachama wake wenye ushawishi kwa nguvu au kwa ushawishi wa fedha na vyeo, kugoma kuwatangaza washindi kwenye chaguzi, kuwapora haki yako ya uchaguzi, kuwabambikia kesi, kuwaua, kuhujumu shughuli za kuwaingizia kipato viongozi wake, na hata kuchafua haiba yao kwenye jamii. Hii ya kuchafua haiba yao ndio akina Paskali wamepewa mchongo, ili wahakikishe CDM inachafuka, kisha itengenezwe justification ya kuwa kwanini CDM imekufa. Kwa sasa kuna mpango wa wazi wa kuifuta CDM, hivyo inatafutwa sababu ili umoja party iweze kuanzishwa na watanzania kushurutishwa kuikubali kwa faida ya CCM. CCM walifanikiwa huko nyuma kwa michezo hii michafu ya kuua vyama pendwa, je wataweza sasa kukiwa na kizazi kipya? Ngoja tuone hii kazi waliyopewa akina Paskali kama watatoboa.
 
Maana wafuasi wa Chadema mnaongoza kumtukana Magufuli huku mkijua hawezi kujibu kwasasa
[emoji15][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji2827] Nadhani hizi ni tuhuma mpya zisizo na ithibati
Magufuli alikuwa hataki kukosolewa, wala mawazo mbadala.Alikuwa bingwa wa kutukana na kuumbua hadharani. Amekufa akiwa kajaa chuki na visasi moyoni mwake.
 
Pasco bana au aliwapelekaea invoice hazikulipwa?
 
SAFI kabisa
 
Good analysis
 
Thanks Tindo kwa uchambuzi wa kina uliobeba dhima ya uhalisia kwa kile kinachoendelea sasa
 
Lakini mama ni rais wako hadi 2030 utake usitake
 
Great sinker theorem
Tabia hii ya mtu akikukosoa unamuona adui ni ya kipumbavu sana!

Eti hadi uzi unaanzishwa ili kumshambulia mtu kisa anaikosoa chadema?

Sasa democrasia mnayoililia kila siku ni ipi? Ni ile ya kuisifia chadema tu?
 
na pale alipominywa kengele Kisha kuitwa mjengoni Dodoma ndipo habari take ilipoishia
 
anakosoa kumshina Pascal Mayalla ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…