CHADEMA imepoteza misingi, Malengo, Uelekeo na Madhumuni ya kuanzishwa kwake

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Abdul mtoto wa Samiah.
 
Huyu Mtoto wa Rais Abdul anacheo gani Kwa watanzania hadi agawe njuruku Kwa kila mtu??
mengune sifahamu,

ila umeshasema mtoto wa rais, hicho ni cheo pia ama haifahamiki?
 
Waasisi wa Chadema walisema Wazi Taasisi yao siyo kwa ajili ya kuongoza DOLA bali kukamata Fursa mbalimbali

Ndio Sababu unaona Mbowe yuko kibiashara zaidi
ooh kumbe?

kwahiyo kinachoendelea kumbe kinaweza kua ni vita ya fursa za deals za tenders mbalimbali ndani ya chama, pesa na mali za chama ee ee
 
Ripoti za CAG kuhusu mismanagement of resources huwa zinahusu Chadema?
 
Ccm ilipoteza malengo misingi ya kuanzishwa kwake 1995 alisema kolimba wakamuua ulikuwa hujazaliwa dogo ccm umeija juzi

Wameendelea kuua wakosoaji akina lowasa, membe nk
 
Chama kimeyumba sana
 
Ccm ilipoteza malengo misingi ya kuanzishwa kwake 1995 alisema kolimba wakamuua ulikuwa hujazaliwa dogo ccm umeija juzi

Wameendelea kuua wakosoaji akina lowasa, membe nk
nyie ndio mnaandikaga matusi kwenye mitihani. sasa sijui ni huwa swali ni gumu au makusudi tu πŸ’
 
Ripoti za CAG kuhusu mismanagement of resources huwa zinahusu Chadema?
si ungekaandikia uzi tuone namna wangwana humu jukwaani wataeleza nini gentleman πŸ’
 
Ndugu mtunga huu Uzi, Naomba nikufahamishe kua wao Chadema wako vilevile katika misingi na lengo la uanzishwaji wake.
Tatizo lipo kwenu mnaoifuatilia Chadema mkidhani itawakomboa kwenye shimo fulani; utitiri wa Kodi, maisha magumu, bei za bidhaa juu, n.k

Wao Chadema ni chama cha siasa ambao shughuli zao siku zote ni siasa tu, hata hayo unayoyadhani kwao hayako sawa sababu ni siasa tu.
 
kwahiyo huna jibu la kisiasa pia, right?πŸ’

by the way mim sio mtunga uzi,
ni kiongozi shupavu wa wananchi, mkufunzi mwandamizi, mwanasiasa na mwanadiplomasia mbobevu, mfanyibiahara, mkulima na mfugaji, lakini pia mtafiti wa masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, kitaifa na kimataifa...

ukiona chochote nimekiwasilisha humu, kaa ukijua tayari nimekifanyia utafiti wa kutosha na kwahivyo najaribu kujiridhisha na kuthibitisha matokeo ya utafiti wenyewe,

hata hivyo,
ikiwa una uhaba wa taarifa kuhusu masula mbalimbali, tafuta maandiko yangu itakusaidia kuongeza uelewa na ufahamu wa kutosha, na kuondoa unyonge ulionao katika kujibu maswali na kuchangia hoja, okay?πŸ’

kuna changamoto chadema gentleman πŸ’
 
si ungekaandikia uzi tuone namna wangwana humu jukwaani wataeleza nini gentleman πŸ’
Nime'pose' tu swali kuhusiana na mada ya ndugu aliyeanzisha mjadala ndugu yangu. Sina upande wowote, ila huwa nataka tuwe fair kila upande.
 
Ni dhahiri unawasilisha mawazo yako unavyoichukulia Chadema na unajikita kwenye kivuli cha mtafiti mbobezi wa Siasa kitaifa na kimataifa.

Lakini ukweli ni kua Tangu vyama vya siasa (mfumo wa vyama vingi) kuanzishwa lengo ni kufanya siasa, si hio dhana yako kwa Chadema au pia vyama vingine vyovyote vya kisiasa.

Hayo unayo yaongelea ni jinsi wewe utakavyo/upendavyo kuhusu chama fulani.
Kumbuka mfumo wa vyama vingi sehemu nyingine ya malengo ni;
1. Kuwawezesha watakaokosa nafasi ya madaraka ndani ya Sisiyemu basi wawanie madaraka nje yake
2. Kutoa nafasi kwa wapiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka (usichanganye na atakaye tangazwa mshindi)

Chadema hawajawahi kwenda nje ya malengo ya kufanya siasa.
 
actually,
nachokiona kwako ni kwasababu,
kwanza wewe ni mwanafunzi wa siasa za vyama vingi, hilo liko wazi, lakini pia wewe ni mshabiki tu wa chadema na kabisaa sio mwanachama wa chadema πŸ’

hivi ni kweli kabisa, miongoni mwa malengo muhimu ya siasa za vyama vingi ni kuwawezesha watakao kosa nafasi za madarakani ndani ya chama A, wakatafute madaraka kwenye chama B? kweli ndrugo zango?🀣

na kama chadema haijawahi kwenda kinyume na malengo yake,
iliwezekanaje kwa mfano, kwa miaka mingi chadema iliimba na kupiga kelele kwamba mtu fulani ni fisadi halafu ghafla mtu huyo huyo akawa mtakatifu tena VIP kwenye chama na kupewa na nafasi ya kugombea urasi wa nchi kabisa dah? nashindwa hata kuendelea aise πŸ’

hivi kweli unaelewa maana ya msingi, malengo na uelekeo?

ile ni siasa au biashara ya siasa na uongozi?πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…