CHADEMA imetulizana, UVCCM wanahangaika kujinasibu kama ACT-Wazalendo

CHADEMA imetulizana, UVCCM wanahangaika kujinasibu kama ACT-Wazalendo

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Unaweza ukaishi kwa mfalme bila amani. Unaweza kuishi kwa mfalme ukawa na hofu hata ya majirani wema wanaoendelea na shughuli zao. Unaweza ukapata fursa ya kumshauri mkubwa akabaki kuwashambulia majirani wanaojiendeleza.

Ndivyo walivyo vijana wa chama tawala, muda walionao wangewekeza kushauri serikali iliyopo madarakani wangeiponya serikali na jamii kwa ujumla.

Naangalia huko mitandaoni vijana wa CCM wote wamekuwa Wana ACT-Wazalendo. Tunajiuliza hizi argument zitajenga madarasa, barabara na zahanati?

Maisha yanaenda kasi sana, kila siku zinavyokwenda ndivyo chama tawala kinapopoteza watu wenye nia yakuwekeza akili zao kuikwamua nchi.

Ukimya wa CHADEMA uwe fundisho kwenu kwamba, busara na makuzi waliyonayo vijana wa CHADEMA pamoja na uwezo wao wakujenga hoja ndivyo vinavyowafanya waaminike na si uwezo wao wakuandika uzushi mitandaoni.
 
Ni ukimya au kunyamazishwa?
Vyovyote utakavyotafsiri ila ukimya ni fimbo kwa madikiteta uchwala. UVCCM wanakesha mitandaoni kuona Lissu ataongea nini! Mtoa post niruhusu andiko lako nilipeleke Twitter karibu na Polepole asome.
 
Back
Top Bottom