CHADEMA inawaza madaraka tu hawana Sera za kukwamua uchumi wa Tanzania

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Sijaona maono yoyote ya maana kutoka kwa Mwenyekiti mpya wa chadema ambayo yanaweza kubadili nchi zaidi ya kuwazia madaraka ya kiserikali tu.

Sijasikia mipango madhubuti kwenye sekta mbalimbali mfano kilimo,teknolojia,ajira,afya,elimu au maswala ya ulinzi na usalama.

Ni ujuha kalulu kufikiri katiba mpya itakupa maswala ya msingi ambayo dunia ya leo inakabiliana nayo.

Marekani ambayo tunaamini ina katiba bora leo hii inapambana na ufisadi kupiti DOGE ya Elon Musk....hii inamaanisha katiba si lolote si chochote inapokuja kwenye swala la ustawi wa nchi na watu wake.

Tuendelee kuiamini CCM na tuipe mambo muhimu ya kufanyia kazi ...tuachane na vibweka vya wapinzani visivyo na muelekeo.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Sasa mtu unaitwa jingalao utaweza kuielewa chadema kweli, wewe size yako ni ccm lumumba buku7
 
Sasa CCM iliyo kaa madarakani miaka zaid ya 60 na wananchi wake wanakunywa maji na mifugo hadi sasa unaisemaje!??
 
Hakuna Chama chenye Sera nzuri kwa maendeleo ya Tanzania hii kama Chadema.

Ili kufanikisha Sera zake lazima washike kwanza dola ( Wapate madaraka) maana hiyo ndo njia pekee itakayowawezesha kutekeleza Sera zao.
 
Ila wanaccm wajue kutokana na kukosekana chama mbadala wawe makini kuteua viongozi wajamaa na wazalendo na wawe tayari kukosoa viongozi wasio na fikraa za kijamaa na wale fisadi. Tumeona ccm wakiwepo vigogo wake waliyofurahia kufa magufuli na mama kuyumba hajitambui kwamba nchi inatakiwa kwenda kwa falsafa ya chama ya ujamaa na kujitegemea.
 
Kwahiyo uneridhika na sisiemu kwa hii miaka zaidi ya 60 ?
 
Utakwamuaje kabla hujapata madaraka,bwana mdogo kaone uso
 
Haya ni maneno ya kawaida ya mwanaccm yoyote.
 
Hakuna Chama chenye Sera nzuri kwa maendeleo ya Tanzania hii kama Chadema.

Ili kufanikisha Sera zake lazima washike kwanza dola ( Wapate madaraka) maana hiyo ndo njia pekee itakayowawezesha kutekeleza Sera zao.
hold on em tuambie hizo sera zake nzuri. Walikua wanapiga kelele decentralization cha ajabu hata kweny chama chao kumbe hio decentralization haipo tuliwasikia kipindi kile kweny chaguz zao sio maneno yetu. Sasa sera ndogo kama hio tu kweny chama imewashinda sasa wataweza kwel kweny nchi
 
Sera za CHADEMA za uraia pacha zitawavutia Watanzania wengi walioko Diaspora kuja kuwekeza nchini.
 
Mkuu katiba mpya ndio msingi wa yote.

Hakuna jambo baya kama kuona mtu ambaye anaelewa mambo halafu kwa makusudi anaamua kupitisha mambo anayoyaelewa!!

Hii haipo kwenye uchawa wala upumbavu!!!
 
Hao walio madarakani wana kila myenzo miaka 60 plus hakuna cha maana walichofanya zaidi kila mtu anahomolaa na familia yake tu.....sio kwa wananchi masikini wale teeee kabisa hakuna anaewajalii.....wao kushinda uchaguzi kutawala kuiba mipesa.....kudanganya umma wananchi masikini hawana elimu
 

Mkuu hii ni falsafa mufilis!! Haitekelezeki kwa nyakati za sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…