CHADEMA inazamishwa na wachumia tumbo wasiotaka mabadiliko kulinda maslahi yao

CHADEMA inazamishwa na wachumia tumbo wasiotaka mabadiliko kulinda maslahi yao

Kanali_

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2018
Posts
6,438
Reaction score
10,180
Nimeona bandiko la ndugu yangu Yericko Nyerere akieleza sababu anazoona yeye zina mashiko za kwanini atamchagua Freeman Mbowe kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na si Tundu Lissu. Pamoja na urefu wa bandiko hilo nimejitahidi kusoma ila mwishowe nimegundua Yericko kakubali kutumika au kulitumikia tumbo lake na si kuandika kwa kuzingatia uhalisia wa hali ya sasa ya chama chao na nini wanahitaji.

Nikuulize swali moja tu ndugu Yericko: nguvu na ushawishi wa chadema ya 2015 ni sawa na chadema ya leo?

Anguko hilo nyie wachumia tumbo hamlioni? Mmeshawahi kufanya research kujua wananchi wanakichukuliaje chama kwasasa au mnakaa maghetton na kuandika magazeti ya kupost JF?

Nikwambie: Huku mtaani chadema imepoteza mvuto na ushawishi kwa vijana na wanawake ambao ndo mtaji mkubwa kisiasa...wengi wanakiona kama chama cha wachumia tumbo na shida ilianzia kipindi kile kapokelewa Lowassa na ikawa kubwa zaidi kwenye hayo mnayoita maridhiano ambayo kiuhalisia ni maridhiano ya kuridhisha matumbo ya viongozi tu! Ilifika kipindi Chadema kikawa chama cha kupambana na watetezi halisi wa maslahi ya wananchi na si kupambana na wakandamizaji wa haki hizo! Kwasasa tumaini pekee lililobaki ndani ya Chadema ni kufumua safu nzima ya uongozi hasa kichwani kabisa (mwenyekiti) na mtu pekee anayeweza kuirejesha Chadema ilee anaweza kuwa Lissu labda na Heche ila hao wengine wote wameshaonesha udhaifu wao mbele ya dola na hawaaminiki. Mkitaka kushupaza shingo shupazeni then mtaniambia baada ya uchaguzi wa 2025.

NB: Kuna namna uongozi wa Chadema chini ya FAM unacheza huu mchezo kwa maelekezo ya Lumumba.
 
Kwasasa tatizo kuu la chadema ni Mbowe, ila kumng'oa hapo ni shughuli kwasabb kajaza michawa na mikunguni ya kutosha hao wajumbe mkutano mkuu hamna kitu pale!.
Wanachama wa kawaida tunguruhusiwa kupiga kura Mbowe asingevuka 30% ya kura zote!!.
Wakimchagua tena mbowe mm ni mmojawapo nitakayeacha kushabikia chadema baada ya miaka kibao ya kufanya hivyo.
 
Ubinafsi ndo unaziharibu taasisi nyingi, Mabadiliko ni muhimu kwa taasisi, nje ya hapo ni changamoto...
 
Leo ndo siku ile ya wajumbe wa mkutano mkuu kuamua wanataka CHADEMA ipi, ya kuwalamba miguu watawala au ya kupambania maslahi ya nchi.
 
Back
Top Bottom