Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
"Mtashurutishwa kutii ratiba, kanuni na sheria za nchi bila shuruti mpaka lini chadema yangu? Vijana wanatukana viongozi wa nchi wanaachwa tu? Nani atatupenda chadema, na nani atatuheshimu sisi kama chadema kwa hali hiyo? Tutaacha kugawanyika kweli kama ndio hivi? nani atachagua watu ambao hawana nidhamu?"
Alifoka kwa uchungu sana mwanachama moja kindakindaki wa Chadema, mtu mzima flani hivi kwenye kijiwe cha kahawa asubuh ya leo.
Kukamatwa kwa viongozi waandamizi wa chadema kila uchwao, inadhihirisha wazi wazi chadema imepoteza uelekeo.
Kauli na maelezo ya viongozi wake waandamizi kwenye kampeni, kunashiria kukata tamaa kwa kiwango kibaya sana.
Kudhihaki na sasa zingine kutukana viongozi wa umma wa kitaifa ndiyo pekee ujasiri waliobaki nao, kitu ambacho kinawakera na kuwaudhi waTanzania wengi na kuwafanya wawachukie na kuwapuuza chadema kwa kiwango cha juu sana. Ni dhahiri hakuna wa kudhibiti utovu wa nidhamu kwa vijana au wazee ambao ni waandamizi ndani ya chadema.
Vilevi wanavyotumia kabla ya kupanda kwenye majukwaa ya kisiasa ili vinawapa ujasiri wa kusema hovyo na kujidhalilisha wao wenyewe, na kupoteza au kudhoofisha kabisa imani za wanachama wao.
Heshima ni kitu cha bure, epuka Kievi kama ndiyo dawa ya kukupa ujasiri wa kuzungumza hadharani, utaumbuka 🐒
Mungu Ibariki Tanzania.