LGE2024 CHADEMA Iringa mjini wasusia Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Iringa Mjini kimesusia uchaguzi wa serikali za mtaa kwa Kilee walichokiita kutoridhishwa na mwenendo mzima wa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini.

Akizungumza na Nuru Fm mwenyekiti wa Chama Cha Dermokrasia Na Mandeleo {Chadema} Jimbo la Iringa mjini Frank Nyalusi amesema kuwa wameamua kuchukua mamuzi hayo kutokana na kutotendwa haki kwa mawakla wa chama hicho kwa kutopokelewa na wengine kunyimwa vibali.

Pamoja na juhudi za msimamizi wa uchaguzi kuruhusu mawakala kusimamia zoezi hilo baada ya majadiliano nyalusi ametaja sababu za mawakala wao kutopigiwa muhuli.

Soma pia: Iringa: RC Serukamba ashiriki zoezi la kupiga kura, asema changamoto ya wakala wa CHADEMA yatatuliwa

Awali mkuu wa mkoa wa iringa akiwa katika kituo chake cha kupigia kura amesema waliamuru kusitisha kwa muda mchache zoezi la upigaji kura ili mawakala wa chadema wagongewe mihuri kwenye fomu zao ili vyama vyote vishiriki uchaguzi.

Itakumbukwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliagiza uchaguzi wa serikali za mitaa ufanyike pasipo vurugu kwa kulinda amani tulionayo huku akitaka wapiga kura waheshimiwe ili kutimiza wajibu wao.

Your browser is not able to display this video.



Chanzo: Nuru FM
Video: Ebony FM
 
Sidhani km hamkujua hayo yatatokea pale mlipokubali kuingia kwenye uchaguzi huku mkijua TAMISEMI ndo wasimamizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…