mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 340
- 359
Miezi zaidi ya mitano sasa inaelekea huku kukiwa na mvutano baina ya CHADEMA na Wanachama wake 19, walio Bungeni kwa sasa.
Chama hicho kila kinapojitokeza hadharani kinaeleza kuwa Wanachama hao wamefukuzwa hivyo hawana sifa ya kuwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wanasema sababu ya kufukuzwa kwao, ni kwenda tofauti na msimamo wa chama wa kutotambua matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Kwamba maazimio na matamanio ya chama hicho ni kubaki wakati wote bila kutambua matokeo ya jumla yaliyowapatia nafasi yoyote ya kiuongozi, kimapato na uwakilishi baada ya oktoba mwaka jana.
Lakini katikati ya hoja yao hiyo, msimamo wao huo haugusi ruzuku zilizotokana na uchaguzi huo. Msimamo wao huo hauwahusi madiwani na Mbunge mmoja waliopata kutokana na Uchaguzi huo.
Na kila wakiulizwa sababu ya kuruhusu madiwani na Mbunge mmoja kuwa halali, na kuwaharamisha wabunge 19, nafasi zilizotokana na uchaguzi huo, huwezi pata jibu sahihi.
Sana sana watakueleza kuwa wamekiuka maagizo ya chama, na ukiuliza ni maagizo gani watakwambia msimamo wa chama ni kutotambua matokeo yoyote ya uchaguzi wa 2020 na kila kilichookana nacho.
Ukiwauliza madiwani na mbunge mmoja nafasi yao ikoje kwenye msimamo huo, watakuambia wao wamechaguliwa na wananchi kwa kura halali ambazo chama kimesusia kwa msisitizo wa kutopeleka viti maalum, yaani ni vurugu tupu maelezo yao.
Kwa msingi huo sasa hata wafuasi na wanachama wa chama hicho hawajui usaliti wa wabunge 19 ni upi na uhalali wa mbunge mmoja na madiwani walioruhusiwa kuapa ni upi. Katikati ya sintifahamu hiyo, watanzania tukaona wameomba fursa ya kukutana na Rais Samia kwa ajili ya kutafuata muafaka.
Watu makini mfano Absalom Kibanda alipowashauri kama wapo radhi kutafuta muafaka waanze na sakata la wanachama wao 19,matusi yakawa mengi, huku hoja ikiwa utaongeaje na wasaliti waliokubali matokeo ya 2020 kinyume na msimamo wa chama.
Jana Mnyika kahojiwa na chombo cha habari anasema ruzuku ya chama hicho haitokani na nafasi ya ubunge wa viti maalum walivyopata chama chake. Hili ni sawa kabisa nami naunga mkono, sasa swali langu kwao je wameanza kutambua uhalali wa matokeo ya 2020?
Je, wamechukua na wanatumia ruzuku iliyotokana na matokeo wasiyokubaliana nayo?
Au wanataka tuamini/niamini yale yanayosemwa katika korido za ofisi mbali mbali za chama hicho, kwamba shida si uhalali wa matokeo, bali shida ni kwanini majina yaliyotakiwa kwenda kutoka kwa baadhi ya viongozi nje ya vikao vya bawacha hayajawekwa katika umafia mzima wa kupeleka majina bungeni.
Au niamini kuwa msimamo wa walioingia bungeni kukataa kuchangia 100m kwa kila mmoja baada ya kuapishwa ndiyo sababu?
Nitarejea