Kigoma kama ilivyo Pemba kwa miaka mingi wamekuwa wanalalamika kwamba wanatengwa na serikali katika kuwapelekea maendeleo,na siyo sasa tuu hata wakati wa mfumo wa Chama kimoja.
Tatizo limeanza pale CHADEMA na CCm kufungana katika idadi ya madiwani wanaotakiwa kuchagua meya na kwa kuwa wanapiga kura kwa kufungamana na chama (Party lining voting) isingewezekana chama chochote kati ya hivyo viwili kushinda
ukapendekezwa muafaka wa kuongoza Halmashauri hiyo kwa kupokezana kwa miaka miwili na nusu kwa kila chama. Sasa zamu ya CHADEMA inakwisha mwezi julai 2008. Ndiyo CCm wana shaka kwamba huenda CHADEMA hawatakabidhi madaraka kwao!
Jambo ninaloliona hapa kwangu ni kwa nini CCM inataka uungwana katika kutekelezwa kwa muafaka wa Kigoma wakati wao hawajawahi kuonyesha hata siku moja uungwana wa kujaribu achilia mbali kutekeleza muafaka wa Zanzibar!