Elections 2010 Chadema iwaambie wananchi haya - pokeeni pesa za CCM ila kura zenu mpige mnakopenda

Solomon David

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2009
Posts
1,148
Reaction score
17
Wengi hapa tumesoma yaliyotokea dodoma kwenye mkutano wa bilal. Jamaa alikosa watu kabisa ikabidi malori yatumike kutafuta watu sehemu zingine na kuwaleta kwenye mkutano (kwa mafungu).

Hawa jamaa kwa kweli pesa wanazo, wamejaza mabango yote Tanzania, waandishi wa habari wote wanalipwa laki kwa siku, TV na radio zote wameweka mfukoni. Na bado wanalipa watu buku moja au mbili kuhudhuria mikutano yao (unakumbuka mkutano wa jangwani?)

CHADEMA haiwezi kupambana na pesa za CCM. Ukichukulia kuwa watanzania wengi ni masikini, wengi wanaridhika tu hata wakipewa elfu moja ya mboga. CHADEMA wakubali tu kuwa hawana pesa za kuwahonga wananchi, hawana pesa za kusambaza mabango nchi nzima (oooppppsss ccm imenunua mabango yote), na hawana uwezo wa kununua vipindi ITV, Star, Channel 10 nk.

CHADEMA iwakumbushe wananchi kuwa upigaji kura ni siri, hakuna mtu atakuja kuchungulia wamempigia nani kura. CHADEMA iwaruhusu wananchi wachukue pesa za CCM lakini kura wapige kule wanakopenda.

CHADEMA iwaruhusu tu wananchi wachukue rushwa (takrima au chochote unachopenda) maana haina uwezo wa kuizuia anyway.

CHADEMA ikiri kuwa haina pesa za kuhonga hivyo wananchi wasisubiria kidogo kidogo toka kwao. Hata hivyo, wapige kura kwa mapenzi yao na si pesa.
 
siku walipozindua kampeni zao, mabasi yote ya dar express na KLM yalikodiwa kuleta watu kutoka mikoani!
 
Kitaalamu ni kwa vipi kusomaba wana CCM kutoka eneo lingine la mkoa au wilaya linaweza kuwasaidia katika kupata kura tunaomba yeyote mwanamageuzi akiona malori wanayobeba wanachama wa CCm kwenda kwenye eneo lingine la kampeni lipigwe picha na kusambazwa katika vyombo mbalimbali ili wananchi wajue zaidi kwamba CCM hawana lao wamekishwa kama matambara mabovu
 
......CHADEMA iwakumbushe wananchi kuwa upigaji kura ni siri, hakuna mtu atakuja kuchungulia wamempigia nani kura. CHADEMA iwaruhusu wananchi wachukue pesa za CCM lakini kura wapige kule wanakopenda.

Wananchi walio wengi huko vijijini uelewa wao wa mambo ni mdogo sana. Akishachukua rushwa ya mtu, anahisi kama vile asipompigia, mtu yule anaweza kujua. Yaani vile virushwa kama T-shirt, Kanga, Kitenge, Kofia, Elfu Mbili, tatu na kadhalika vinawafanya watu wanakua ''loyal'' kwa aliyewapa na mara nyingi huwa hawawaangushi hawa watoa rushwa.

CHADEMA wanaweza kulisemea hili kwenye kampeni zao (japo dakika chache kabla ya kumaliza hotiba) na kutoa elimu kidogo kwa raia. Kama mtu analetwa rushwa, chukua hiyo na siku ya uchaguzi chagua CHADEMA. Aliyetoa rushwa atajua kaliwa siku matokea yakitoka ila hatoweza kujua nani na nani hawakumchagua. Ni muhimu Mama/Dada/Bibi na babu zetu kule vijijini wakalielewa hili
 
Tusaidie kuwaelimisha.

Kwa vyovyote mtu kama hana hata tsh 500, ghafula anatokea mtu wa kumpa 2000 atafurahi sana. Ila waambiwe hizo hela za CCM wachukue tu ni kodi za wananchi walizoiba. Ila wasiziuze kura zao kwa gharama yoyote ile, kwani siku ya kupiga kura ni siri.

Kura zote ziwe kwa mgombea Makini sio kwa wababaishaji wa CCM hasa JK.
Sina chuki na JK ila hana uwezo. Sio vizuri kuendelea kumbebesha mzigo ambao yeye mwenyewe kashaonesha kuwa hawezi.
 
CHADEMA iwakumbushe wananchi kuwa upigaji kura ni siri, hakuna mtu atakuja kuchungulia wamempigia nani kura. CHADEMA iwaruhusu wananchi wachukue pesa za CCM lakini kura wapige kule wanakopenda.

CHADEMA iwaruhusu tu wananchi wachukue rushwa (takrima au chochote unachopenda) maana haina uwezo wa kuizuia anyway.

CHADEMA ikiri kuwa haina pesa za kuhonga hivyo wananchi wasisubiria kidogo kidogo toka kwao. Hata hivyo, wapige kura kwa mapenzi yao na si pesa.
Pathetic
 
Wengi hapa tumesoma yaliyotokea dodoma kwenye mkutano wa bilal. Jamaa alikosa watu kabisa ikabidi malori yatumike kutafuta watu sehemu zingine na kuwaleta kwenye mkutano (kwa mafungu).

Hawa jamaa kwa kweli pesa wanazo, wamejaza mabango yote Tanzania, waandishi wa habari wote wanalipwa laki kwa siku, TV na radio zote wameweka mfukoni. Na bado wanalipa watu buku moja au mbili kuhudhuria mikutano yao (unakumbuka mkutano wa jangwani?)

CHADEMA haiwezi kupambana na pesa za CCM. Ukichukulia kuwa watanzania wengi ni masikini, wengi wanaridhika tu hata wakipewa elfu moja ya mboga. CHADEMA wakubali tu kuwa hawana pesa za kuwahonga wananchi, hawana pesa za kusambaza mabango nchi nzima (oooppppsss ccm imenunua mabango yote), na hawana uwezo wa kununua vipindi ITV, Star, Channel 10 nk.

CHADEMA iwakumbushe wananchi kuwa upigaji kura ni siri, hakuna mtu atakuja kuchungulia wamempigia nani kura. CHADEMA iwaruhusu wananchi wachukue pesa za CCM lakini kura wapige kule wanakopenda.

CHADEMA iwaruhusu tu wananchi wachukue rushwa (takrima au chochote unachopenda) maana haina uwezo wa kuizuia anyway.

CHADEMA ikiri kuwa haina pesa za kuhonga hivyo wananchi wasisubiria kidogo kidogo toka kwao. Hata hivyo, wapige kura kwa mapenzi yao na si pesa.

Hapa Umenena Mkuu, walio karibu na DR. Slaa na timu yake ya kampeni huko mikoani plse! plse! mkumbusheni awaambie watu hili jambo ni muhimu sana.
CCM wana kila kitu na wanajua maji yapo shingoni sasa wanapanga mbinu wanazo nyingi sana lazima CHADEMA wawe macho kukabiliana nao.
 
Wananchi walio wengi huko vijijini uelewa wao wa mambo ni mdogo sana. Akishachukua rushwa ya mtu, anahisi kama vile asipompigia, mtu yule anaweza kujua. Yaani vile virushwa kama T-shirt, Kanga, Kitenge, Kofia, Elfu Mbili, tatu na kadhalika vinawafanya watu wanakua ''loyal'' kwa aliyewapa na mara nyingi huwa hawawaangushi hawa watoa rushwa.

CHADEMA wanaweza kulisemea hili kwenye kampeni zao (japo dakika chache kabla ya kumaliza hotiba) na kutoa elimu kidogo kwa raia. Kama mtu analetwa rushwa, chukua hiyo na siku ya uchaguzi chagua CHADEMA. Aliyetoa rushwa atajua kaliwa siku matokea yakitoka ila hatoweza kujua nani na nani hawakumchagua. Ni muhimu Mama/Dada/Bibi na babu zetu kule vijijini wakalielewa hili
Wala si vijijini pekee, hata mijini hususan hapa Dar wapo ambao ni mbumbumbu vile vile hawaelewi tofauti ya ndewe na sikio! Wao ni bendera yafuata upepo wanaishi maisha ya dhiki wao na familia zao lakini wanaamini kwamba maisha hayo ndiyo sahihi wala ukiwaeleza kwamba yanaweza kubadilika kwa kuwepo uongozi bora, hawakuelewi na wengine wanaweza kukubishia na kusisitiza kwamba wao ni CCM tu mpaka ukabaki mdomo wazi!

Kampeni za kuwaelimisha wananchi inabidi ziwe endelevu hata baada ya uchaguzi vyama vya upinzani viendelee kuwaelimisha wananchi kwamba CCM si baba wala mama yao mzazi!
 
uko sawa kabisa mkuu,ikiwezekana wafanye demo ya kupiga kura halafu badaye mtu apewe kazi ya kutambua ya kwake.
 
Wengi hapa tumesoma yaliyotokea dodoma kwenye mkutano wa bilal. Jamaa alikosa watu kabisa ikabidi malori yatumike kutafuta watu sehemu zingine na kuwaleta kwenye mkutano (kwa mafungu).

Hawa jamaa kwa kweli pesa wanazo, wamejaza mabango yote Tanzania, waandishi wa habari wote wanalipwa laki kwa siku, TV na radio zote wameweka mfukoni. Na bado wanalipa watu buku moja au mbili kuhudhuria mikutano yao (unakumbuka mkutano wa jangwani?)

CHADEMA haiwezi kupambana na pesa za CCM. Ukichukulia kuwa watanzania wengi ni masikini, wengi wanaridhika tu hata wakipewa elfu moja ya mboga. CHADEMA wakubali tu kuwa hawana pesa za kuwahonga wananchi, hawana pesa za kusambaza mabango nchi nzima (oooppppsss ccm imenunua mabango yote), na hawana uwezo wa kununua vipindi ITV, Star, Channel 10 nk.

CHADEMA iwakumbushe wananchi kuwa upigaji kura ni siri, hakuna mtu atakuja kuchungulia wamempigia nani kura. CHADEMA iwaruhusu wananchi wachukue pesa za CCM lakini kura wapige kule wanakopenda.

CHADEMA iwaruhusu tu wananchi wachukue rushwa (takrima au chochote unachopenda) maana haina uwezo wa kuizuia anyway.

CHADEMA ikiri kuwa haina pesa za kuhonga hivyo wananchi wasisubiria kidogo kidogo toka kwao. Hata hivyo, wapige kura kwa mapenzi yao na si pesa.
Hii yako ni nzuri.....lakini hapo kwenye nyekundu pananitatiza kidogo. Ina maana CHADEMA wangekuwa na pesa nao wangehonga?? Kama ujumbe unaotaka kuutoa ni kuwa CHADEMA haitaki kujihusisha kwa namna hii, expression ya "haina pesa za kuhonga" isomeke "haina roho (spirit, sera, etc) ya kuhonga". Au??
 
Whatever jina ccm wanatumia - takrima, shukrani, pesa ya maudhurio, etc, hii ni hongo na inabidi itajwe hivyo.
 
Back
Top Bottom