Uchaguzi 2020 CHADEMA jipangeni kwenye kuandaa mikutano

ndomyana

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
5,630
Reaction score
2,169
Nimeshangaa na kukurupuka kwa chama hiki kuandaa mkutano wa leo Zackem, Mbagala. Maandalizi mabovu watu wa Dar wanahitaji uwaandae uwape muda wakuweke kwenye ratiba.

Dar sio mkoani au wilayani ambako watu wanaweza kusanyika kirahisi kwa muda mfupi. Hili tukio lilipaswa liwe maalumu kwa siku maalumu ya wikiend kama kesho. Sasa ndugu zangu ghafla tu ona mahudhurio hafifu na ujumbe haujafika, mmewapa wenzenu cha kuongea. Siku ya ufunguzi ilipaswa iache historia.

Jipangeni kama hamuwezi jipanga kuandaa mikutano kama zamani mtaweza linda kura kama mnavyodai?

Nimehudhuria mikutano mingi ya CHADEMA Arusha NMC Mbeya Rwanda nzovwe, Dar Jangwani ilijaa watu. Sio kama wa leo japo nyomi haipigi kura ila inatia moyo.
 
Kibaya zaidi hakuna Cha Maana walichoongea zaidi ya kulialia na kulazimisha kuwachangisha wananchi pasipo hiari Yao, heti "chukua simu bonyeza *150*00# na blaaablaa kisha weka kiasi" Huu Ni utapeli Tena wa waziwazi.

Haya baada ya kuona zoezi la kuwatapel pesa zao wananchi kupitia simu wakaamua kupitisha makontena ya kuchangia pesa nayo yakabuma wananchi wakawaruka.

Kwa vitendo baadhi tu hivi vya leo hakika mikutano Yao imepoteza mvuto kabisa na wananchi watakuwa wanaziogopa Sana maana wao wanaenda kwaajili ya kusikiliza Sera matokeo yake wanaenda kulazimishwa kuchangia Tena kwa njia ambazo siyo za hiari Wala arifu.

 
Kumbe leo ni siku ya kazi [emoji23][emoji23] chadema mmedoda msijitetei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…