Hivi mgombea wa CCM kula hindi la kuchoma hadharani ndiyo "seriousness" ya mgombea wa kiti cha Urais inavyotakiwa?CCM ndio walio serious na maisha ya Watanzania?
Well said 👋 👏Mkuu kwanza kampeni bado hazijaanza kwa hiyo hayo mambo yataongelewa huko.
Pia kuna issues ambazo hazina sura ya kutaifa hivyo si muhimu ziongelewe popote pale mfano ukimuongelea korosho mtu wa kanda ya ziwa ataona ni jambo la maana kwake? Vitu kama hivyo vitaongelewa huko sehemu husika.
Kwa hiyo Jpm anapambana na rushwa? Kutumbua watu hovyo hovyo kwa tuhuma za ubadhirifu na kisha baadae kuwarejesha bila hatua yoyote kuchukuliwa kwako ndio mapambano ya rushwa?
Kama anapambana na rushwa kwa nini hataki miradi aliyoifanya bila idhini ya bunge isikaguliwe, anaficha nini? Kwa nini amuondoe CAG (Assad) baada ya ripoti yake kuonesha deficit ya 1.5trl badala ya kushughulikia huo upotevu?
Nini ambacho mwananchi wa kawaida amesaidiwa na kikapondwa? Mfano katumbua watu wenye vyeti feki kisha kamuacha Makonda anayetuhumiwa kwa kosa hilo hilo tena anasema mradi anachapa kazi hata kama hana vyeti, huyo ndio mtu anaye wasaidia wananchi?
Mwisho huu ni uchaguzi, anayeona ana sababu za kumchagua huyo magufuli na akamchague na watakao shawishiwa na Lissu nao watampigia kura pia.
Kama yanayosemwa ni uongo kinachotakiwa kwa upande mwingine ni kuusema ukweli, kwanini hawatoi matokeo ya uchunguzi.Muda utasema... Uongo una mwisho, CHADEMA wanauhadaa ulimwengu kuhusu issue ya Lissu. Lakini kilichotokea kinajulikana na hao Viongozi wao wanaujua ukweli lakini baada ya mambo kuwa kinyume tukio hilo limegeuzwa kuwa mtaji. Naamini hata Lissu mwenyewe anajua lakini hana ujanja kwake imekua political gain
Hujui maana ya sera.Sera za Lissu
-Safari hii uhuni basi
-Nikishindwa uchaguzi naingia barabarani
-CCM hawana marafiki
-Magufuli alinunua jogoo kwa tsh 100,000/=
Eee Mwenyezi niweke hai hadi tarehe 28/10/2020 nifanye yangu .
Hata waliokuwapo nchini walizuiwa kuongelea siasa hadi waliporuhusiwa juzi kwenye uzinduzi wa jengo la Tume ya Uchaguzi hapa Dodoma. Kwani hukumbuki juzi tu kwenye vikao vya kuwapata wagombea, kuna watu walikamatwa kwa kufanya vikao vya ndani? Hoja yako ya kutokuwapo kwake nchini haina nguvu hapoKwa kuwa hakuwepo nchini kwa muda mrefu tofauti na wale wengine, inaweza kuwa sababu ili afahamike.
Two wrongs don't make a right 😕 😒CCM ndio walio serious na maisha ya Watanzania?
Wale political scientists wa Chadema akina Professor Baregu wamepuuzwa au Lissu kaja na washauri wapya?Tangu Lisu amerudi siku zote anaongea pumba tu. Hajawai ongea jambo la maana.
Kabisa kabisaCCM ndio walio serious na maisha ya Watanzania?
Hakuna mtu atamipigia kura Lissu kisa kupigwa risasi!. Never atafute hoja mbadala , aongolee issues sio kutafuta kura za huruma kipitia risasi . Wananchi watampa kama ataeleza atafanya Nini cha zaidi ya alicho fanya JPM.Kuna mambo mengi yatakayochangia kumpa Lissu kura, na mojawapo ni hilo shambulio, na sijui kwanini hupendi kusikia kuhusu lile shambulio dhidi yake.
Hakuna tume brotherHilo linaweza kuwepo tena uchaguzi ujao wa 2025