Pre GE2025 CHADEMA kanda ya kati yadai walimu walipewa hela kushiriki sherehe za CCM

Pre GE2025 CHADEMA kanda ya kati yadai walimu walipewa hela kushiriki sherehe za CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati, kimekemea vikali kitendo kinachodaiwa kufanywa na Maafisa Elimu cha kuwalazimisha walimu kwenda kushiriki sherehe ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dodoma tarehe 05 Februari 2025.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Masonga Emmanuel, Maafisa hao wamewafuata watumishi hao wa umma kwa magari na kuwapa fedha za malazi.

Soma Pia:
“Haya ni matumizi mabaya ya madaraka, kuwalazimisha watumishi wa umma kuwa na mlengo wa kisiasa na kutumia kodi za Watanzania na uhuru binafsi wa wafanyakazi kushiriki matukio ya chama kimoja kwa kutumia ushawishi wa madaraka na fedha za walipa kodi wa nchi hii”, imeeleza taarifa hiyo.
 
Back
Top Bottom