Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi, Rhoda Kuchela amebainisha kutokea kwa kasoro nyingi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo Novemba 27, 2024.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Kashato, Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi amesema kitendo cha kuondolewa Wagombea walioapa kama Mawakala kwenye vituo vya Kupigia Kura vinavunja Kanuni za Uchaguzi huo na kufifisha uwazi.
Hivi hawa Wakurugenzi wa hizi Halmashauri ambao ndio wasimamizi wa huu UCHAFUZI ohoo sorry UCHAGUZI , wanashindana kufanya unyama na ukatili kwa vyama pinzani?..na kuna NISHANI kwao?