ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Tukio hilo limetokea hapo jana Julai 18, 2024 kwenye kikao cha baraza la mashauriano la chama hiko lililofanyika katika ukumbi wa Anglican mjini Kasulu mkoani Kigoma.
Licha ya wenyeviti hao kutoa ushauri lakini mwenyekiti Bujoro aliendelea na msimamo wake wa kupinga kuthibitishwa kwa katibu huyo wa mkoa ambaye vikao vya Kanda ya Magharibi vilimpitisha.
Baadhi ya wenyeviti wa majimbo na wilaya za Mkoa wa Kigoma wakiongea kwa nyakati tofauti na Jambo TV wameelezea kuwa, huenda mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kigoma akawa na ajenda yake nyuma ya pazia ikiwemo kutumika kukihujumu chama hiko kuelekea chaguzi za serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani 2025.
Hata hivyo, msimamo wa wenyeviti wa wilaya na majimbo Mkoa wa kigoma wamesema, watasimama na maamuzi ya kamati tendaji ya Kanda ya Magharibi na wataendelea kumtambua Bw. Boniphace Chuzura kuwa katibu wa CHADEMA wa Mkoa wa Kigoma.
See translation
===
My Take
Naungana na Rais Samia aliposema Hawa watu ni Wachanga sana kwenye Uongozi ngoja walelewe wake na wajifunze kwa CCM.👇👇
View: https://www.instagram.com/reel/C9mdzfOBnuM/?igsh=MTZqb2Jua3g5eTNkdg==