Pre GE2025 CHADEMA Kufanya Mikutano 105 kwa siku 21 tu Kanda ya Kaskazini, Lissu na Mbowe kuongoza Mashambulizi

Pre GE2025 CHADEMA Kufanya Mikutano 105 kwa siku 21 tu Kanda ya Kaskazini, Lissu na Mbowe kuongoza Mashambulizi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hii ndiyo Taarifa Mpya ya sasa kutoka kwa Viongozi wa Kanda hiyo

Zaidi soma hapa

Screenshot_2024-06-20-20-38-28-1.png

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatarajia kufanya mikutano 105 katika mikoa minne ya Kanda ya Kaskazini katika Operesheni yake ya kukijenga chama huku wakitarajia kutumia ndege ‘chopa’ katika ziara hizo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Juni 20, 2024, Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa amesema mikutano hiyo itafanyika katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Manyara, Tanga na Kilimanjaro.

Amesema operesheni hiyo ya siku 21 itafanyika katika majimbo 35 yaliyopo kwenye mikoa hiyo na itaongozwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe.

Amesema katika majimbo ya Ngorongoro na Karatu kutafanyika mikutano mitano kila jimbo na itaongozwa na Mwenyekiti Mbowe na Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Tundu Lissu.

"Kwa majimbo ya Ngorongoro na Karatu tunatarajia kufanya mikutano mitano katika majimbo hayo, na kwa upekee Mwenyekiti wa Taifa atashirikiana na Makamu Mwenyekiti Lissu," amesema.

Golugwa amesema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza Juni 22, 2024 katika Jimbo la Karatu mkoani Arusha, ambapo katika majimbo mengine itaongozwa na Mbowe na Mwenyekiti wa Chadema Kanda hiyo, Godbless Lema.

Aidha, amesema kwa sasa wanaendelea kukamilisha maandalizi ya operesheni hiyo ambayo pia watatumia chopa.

"Kaulimbiu yetu tunataka kuonyesha CCM na wapinzani wetu wengine na Watanzania kwa ujumla kwamba tuna watu, tuna Mungu, tuna nguvu. Hiyo ndiyo fahari yetu na uimara wetu Kanda ya Kaskazini ambayo ni ngome ya Chadema," amesema na kuongeza,

"Tunaendelea na maandalizia ikiwemo kupeleka barua ya vibali vya mkutano, ndege kuruka na masuala mengine,"

Katibu huyo amesema operesheni hiyo inafanyika baada ya kumaliza vikao vya mashauriano ndani ya chama vilivyofanyika katika mikoa hiyo ya Kanda ya Kaskazini.

PIA SOMA
 
Tundu Lissu na Mbowe tena,si maccm wamesema hao wameshavurugana hata salamu hawapeani?

Hao ukiwasikia wanaongea chochote kuhusiana na CHADEMA, wapuuze, maana wakati wote wanaongea yaliyomo vichwani mwao au wanayotaka yatokee, na wala siyo ukweli wa yale yaliyopo.
 
Shetani hajawahi kumshinda Mungu
Maarifa nayo ni muhimu sana...mimi huwa siiamini sana chopa .ukizingatia sio mpya sana hadi kuiamini kiasi kuikabidhi watu muhimu kwa taifa hili...according to ngedere1
 
Back
Top Bottom