mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Kama Watanzania walivyotegemea viongozi wa CHADEMA wasingeweza kukaa kimya kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu, uliopangwa kufanyika Jumatano, tarehe 28/10/2020. Hii inatokana na ukweli kwamba Mgombea Urais kupitia hicho chama ameonya, mara kadhaa, kwenye kampeni zake kuwa kama hatatangazwa yeye mshindi, anawambia wanachama, wafuasi na mashabiki wake waingie barabarani. Amekuwa akisisitiza kuwa ama zake ama za Magufuli, mgombea Urais kupitia CCM.
Kutokana kauli ya iliyomo kwenye "video clip" ya Mbowe (naambatanisha), akiwaambia Watanzania kwa njia ya mkutano wake na Wanahabari, kimsingi masharti ya kukuubali matokeo yako mikononi mwa Tume ya Uchaguzi kukubali, bila masharti yoyote, mawakala wa CHADEMA, itakao wateua, kusimamia zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumulisha kura.
Je, ni mazingira gani Mawakala wa CHADEMA wamewekewa na kuandaliwa na chama ili wawe na sifa zinazokidhi Maadili ya Uchaguzi Mkuu, 2020? Moja ya wajibu wa chama cha siasa kinachoshoriki katika Uchaguzi Mkuu, 2020, Kifungu 2.1(r) uwaelimisha na kuwaelekeza mawakala wao watakaokuwepo katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, kanuni za uchaguzi, taratibu na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Angalizo langu: kuna kila dalili, kutokana na historia ya ushiriki wa CHADEMA, kuwa Mawakala watakaoteuliwa watakuwa hawana sifa za kuwa mawakala ili waenguliwe. Ikitokea hivyo chama kitakuwa na sababu ya kususia matokeo. Chondechonde viongozi wa CHADEMA kama lengo ndilo hilo, hakika nawaambia hamna nia njema ya kuongoza nchi hii ila kutafuta kila aina ya uovu nchi isitawalike, mkidhani ikiwa hivyo mtaingia madarakani.
NAWASILISHA