Uchaguzi 2020 CHADEMA kukubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Kama Watanzania walivyotegemea viongozi wa CHADEMA wasingeweza kukaa kimya kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu, uliopangwa kufanyika Jumatano, tarehe 28/10/2020. Hii inatokana na ukweli kwamba Mgombea Urais kupitia hicho chama ameonya, mara kadhaa, kwenye kampeni zake kuwa kama hatatangazwa yeye mshindi, anawambia wanachama, wafuasi na mashabiki wake waingie barabarani. Amekuwa akisisitiza kuwa ama zake ama za Magufuli, mgombea Urais kupitia CCM.

Kutokana kauli ya iliyomo kwenye "video clip" ya Mbowe (naambatanisha), akiwaambia Watanzania kwa njia ya mkutano wake na Wanahabari, kimsingi masharti ya kukuubali matokeo yako mikononi mwa Tume ya Uchaguzi kukubali, bila masharti yoyote, mawakala wa CHADEMA, itakao wateua, kusimamia zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumulisha kura.

Je, ni mazingira gani Mawakala wa CHADEMA wamewekewa na kuandaliwa na chama ili wawe na sifa zinazokidhi Maadili ya Uchaguzi Mkuu, 2020? Moja ya wajibu wa chama cha siasa kinachoshoriki katika Uchaguzi Mkuu, 2020, Kifungu 2.1(r) uwaelimisha na kuwaelekeza mawakala wao watakaokuwepo katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, kanuni za uchaguzi, taratibu na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Angalizo langu: kuna kila dalili, kutokana na historia ya ushiriki wa CHADEMA, kuwa Mawakala watakaoteuliwa watakuwa hawana sifa za kuwa mawakala ili waenguliwe. Ikitokea hivyo chama kitakuwa na sababu ya kususia matokeo. Chondechonde viongozi wa CHADEMA kama lengo ndilo hilo, hakika nawaambia hamna nia njema ya kuongoza nchi hii ila kutafuta kila aina ya uovu nchi isitawalike, mkidhani ikiwa hivyo mtaingia madarakani.

NAWASILISHA
 
Ninachokiona Time atakuwa mtu wa kwanza na wa mwisho kutunza amani ya Tanzania. Kwa Hali ilivyo CCM wakifanyiwa figisu hawatakubali halikadhalika, CHADEMA wakifanyiwa figisu hawatakubali.

Hivyo Kama tume watakosa ueledi na kuamua kupendelea upande mmojawapo Mwaka huu tutegemee ya Kenya 2007.

Ombi kwa tume yetu ya uchaguzi. Tunatambua mnapenda kulinda ajira zenu, lakini sio kwa damu za watanzania. Tuweke professionalism mbele na maslahi ya taifa mbele. Bora kuwa shahidi kuliko mtuhumiwa
 
Uchaguzi unaendeshwa kwa misingi ya sheria, kanuni na maadili ya uchaguzi. Uchaguzi hauendeshwi kwa amri na matakwa ya Mbowe.
 
Ninachokiona Time atakuwa mtu wa kwanza na wa mwisho kutunza amani ya Tanzania. Kwa Hali ilivyo CCM wakifanyiwa figisu hawatakubali halikadhalika, CHADEMA wakifanyiwa figisu hawatakubali...
CHADEMA hawana uwezo wa kuleta fujo.
Majority ni CCM
 
Hilo hata asingelisemea, liko wazi, Magufuli anachukua nji mapema Asubuhi na ushindi wa Magufuli utawalazimisha tu kukubali, maana ushindi wake si cha mtoto
 
Wewe wacha ujinga , waambie tume iwaapishe mawakala , iwape barua za uteuzi , ihakikishe inawapa nakala za matokeo yote ktk kituo udiwani , ubunge na urais , halafu zoezi la upigaji kura , kuhesabu ,kujumlisha , Kutangaza matokeo like la wazi Kama kikao chenu mkutano mkuu CCM ndio watu tutakubali matokeo , tofauti na hapo hakuna .
 
Kama Watanzania walivyotegemea viongozi wa CHADEMA wasingeweza kukaa kimya kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu, uliopangwa kufanyika Jumatano, tarehe 28/10/2020. Hii inatokana na ukweli kwamba Mgombea Urais kupitia hicho chama ameonya, mara kadhaa, kwenye kampeni zake kuwa kama hatatangazwa yeye mshindi, anawambia wanachama, wafuasi na mashabiki wake waingie barabarani. Amekuwa akisisitiza kuwa ama zake ama za Magufuli, mgombea Urais kupitia CCM.

Acha kujifunza kuwa na akili ndogo, weka clip iliyo na maneno yenye rangi nyekundu hapo juu. Nie ndio mnaochonganisha jamii ya watanzania
 
Usimlishe maneno. Alisema kama kutakuwa na wizi hapo ndo atawaambia watu waingie barabarani. Hakusema kama hawatawatangaza. Mbona mnapotosha nyie wahuni wa CCM
 
Hilo hata asingelisemea, liko wazi, Magufuli anachukua nji mapema Asubuhi na ushindi wa Magufuli utawalazimisha tu kukubali, maana ushindi wake si cha mtoto

Sio kwa kura, bali kwa kutegemea tume isiyo huru ya uchaguzi.
 
Taarifa uliyotoa inadhihirisha kweli uwezo wako wa kufikiria uko kunako Masaburi,kwa sababu Mh Lisu hakusema kwamba;yeye alipotangaza ataongoza watu barabarani.

Ila alisema,ikiwa atashinda uchaguzi,tume ikagoma kumtangaza basi ataongoza watu barabarani.

Unapofanya kusema uwongo basi uwe unatumia akili na si vinginevyo
 
Alisema kama akishinda na asitangazwe kuwa ameshinda na wala hajawahi kusema kuwa asipotangazwa kuwa mshindi, usimlishe maneno.
Bwana Sallu, naona kama tunakosea sana, na kupoteza muda kwenye nyuzi za
Kijinga jinga, za watu kama huyu na kina Wakudadavuliwa, bia yetu, Yehoyada nk!

Hawa ni wash Abi li was ujinga na wachochozi wa kudumisha uongo! Ni wapotosha wajinga zaidi kuwepo hapa!
Wamezushia Lisu na CHADEMA uongo mwingi tu, ambao naamini hata watoto wao wachanga, (kama wanao) hawawezi kuukubali!

Hayo yote ni kawaida tu, lakini kero kubwa ni kwamba, kazi hii wanayo fanya, (ambayo haina viwango), wanalipwa🤩, lakini mbaya zaidi wanalipwa na kodi zetu😔😣😭! Bashiru na Polepole ni wahujumu uchumi, peleka mahakama ya mafisadi!!😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…