Uchaguzi 2020 CHADEMA kwa siku 20 hakikisheni mnanyoosha suala la mawakala

onjwayo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2020
Posts
1,356
Reaction score
1,309
Suala la mawakala ni muhimu Sana kwa vyama vya upinzani. Toeni elimu kwa mawakala wenu na ikibidi wachagueni walio watiifu na waadilifu kufanya shughuli ya kusimamia kura zenu. Kila Mara vyesi baada ya matokeo ni njama za kupindisha matokeo.

Kuna rafiki zangu Fulani wamenitonya kuwa kuna fununu kuwa makatibu wa chama fulani wanajaribu kuingilia uchaguzi huu ili kulazimisha wasimamizi wakuu kuwatangaza wagombea wa chama chao hata Kama hawatashinda. Ni habari mbaya na kwa sababu Ni fununu Basi isipuuzwe.

Uchaguzi ukiwa huru na haki, maendeleo ya kweli yatapatikana. Dalili mbaya Ni sawa na Tambo la OCD wa Hai kwa Mbowe kuwa hawezi kumshinda mpinzani wake hata afanyeje. Kama huyu tayari amevujisha Siri Basi kwingineko Hali inaweza kuwa Ni hiyo Kama tahadhari haitachukuliwa. Sasa Ni muda wa kuchuja nani awe wakala atakayesimamia haki kwenye kituo Cha kupigia kura na majumuisho katani na majimboni.

NEC ijaribu kuwa wakweli katika kutoa matokeo na kamwe wasizibe pamba masikioni. Uchaguzi ni gharama kwahiyo kutumia fedha za wananchi kumtengenezea mtu mmoja ushindi Ni kosa la hujumu uchumi.
 
Ukweli unabaki ukweli tu, hata CHADEMA ikipewa haki zote za kusimamia mchakato wa Uchaguzi, hakuna shaka kitashindwa vibaya sana. Sababu ziko nyingi km:
√ wafuasi humu wanashabikia matukio badala ya kutetea Sera ya chama ili wanaJF washawishike na kushawishi ndugu na rafiki zao kukipa kura za kutosha;
√ mgombea Urais naye badala ya kueleza kwa ufasaha Sera za chama, kama zilivyoainishwa kwenye Ilani, anatumia muda mwingi wa muda wake wa kampeni kumdharilisha Magufuli, mgombea Urais kupitia CCM, lakini pia ni M/Kiti wake na Rais wa JMT. Kitendo hicho hakimdharilishi Magufuli kama Magufuli bali Taasisi ya Urais na CCM. Wenye kujua na kuheshimu Taasisi ya Urais na wanachama, wafuasi na mashabiki wa Magufuli, na hasa wanachama wa CCM ambao kwa ujumla wao ni zaidi ya wanachama wa vyama vyote na ni zaidi ya 50% ya waliojiandikisha kupiga kura;
√ mgombea Urais anatoa tuhuma zenye uzushi kumfitinisha mgombea Urais kupitia CCM asijue kuwa nyuma yake akiondoka anaacha ombwe la kutetea uzushi wake maana zinajibiwa na wagombea ubunge na udiwani kwa ushahidi na ushuhuda wa wananchi wenyewe.

Yako mengi yenye kukiondoa CHADEMA kwenye ulingo wa siasa baada ya Uchaguzi Mkuu.
 
Crap
 
Back
Top Bottom