Baadhi ya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Makete mkoani Njombe wamezungumzia uchaguzi wa viongozi wa chama hicho taifa pamoja na namna uchaguzi huo ulivyofanyika
"Siasa za nchi yetu kwa sasa zinamfaa mtu kama Tundu Lissu, Mbowe tunamheshimu sana lakini tumeona apumzike kwa sasa kijiti kipokelewe na mtu mwingine, tumeamua tubadili gia ya gari" amesema Kevin Sanga mwanachama wa CHADEMA.