Chadema mbona hawaeleweki kwenye suala la Katiba, mwanzo walitaka serikali tatu sasa hivi hawataki

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2011
Posts
6,764
Reaction score
896
Wana JF,

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wanawachanganya watanzania kutokana na msimamo wao kwenye suala la Katiba ya nchi, mwanzo walitaka serikali tatu, Tume ya Katiba kwenye rasimu yao wamependekeza serikali tatu, ukiwasikiliza viongozi wa Chadema sasa hivi tena hawataki serikali tatu wanataka serikali mbili au moja.

Hapa chini viongozi wa Chadema wakipeleka mapendekezo yao ya Katiba,

 
Wameshatoa official statement yao baada ya rasimu kutoka, au umeamua kuwawekea maneno yako midomoni mwao? CCM wao wametoa official statement yao kupitia kwa Kinana.
 
Acha u.ji.nga wewe..umeona wapi official statement ya Chadema kuhusu rasimu? Labda nikukumbushe tu kwasababu uko pembezoni: Kinana,Sitta,Ndugai n.k wako CCM (Chama Cha Zamani) na ndo waliotoa matamko kuipinga!
 
Acha u.ji.nga wewe..umeona wapi official statement ya Chadema kuhusu rasimu? Labda nikukumbushe tu kwasababu uko pembezoni: Kinana,Sitta,Ndugai n.k wako CCM (Chama Cha Zamani) na ndo waliotoa matamko kuipinga!

Sidhani kama kuna ujinga hapo nadhani umeyasoma mapendekezo ya Chadema sijui kama waliwashirikisha wanachama wao.
 
Wale wote wanapinga serikali tatu hakiwemo Mzee Mwanakijiji, walikuwa wapi kuwapinga Chadema.
 
Last edited by a moderator:
cdm imepata almost kila kitu walichokitaka kuanzia serikali tatu mpaka idadi ya mawaziri wamechukua namba yao ile ile waliyoitaka cdm kwahiyo Prof.Baregu was right alipowaambia cdm kusubiri mambo mazuri yaja. Tume imeifanya safari ndefu ya cdm kuwa fupi. cdm iweke majeshi yake sawa kwa ajili ya uchaguzi ujao ili waweze kumalizia ngwe ya safari yao.

suala la seriakli ya majimbo ni muhimu kwani inaongeza uwajibikaji ikitokea upungufu wa askari mtaani kwako mnashinikiza jimboni kwako na unajua wazi uende ukambane nani na huyo mtu mhusika anajua hasiposhugulikia tatizo hilo nini kitamfika wakati wa uchaguzi kuliko hali ya hivi sasa ambapo itambidi kila mtu nchi nzima aende dsm kumtafuta nchimbi alipo km utampata na hawajibiki kukusaidia kwani hata km asipokusaidia hakuna namna yeyote ile unaweza kumwajibisha au kufanya lolote lile plus too much power has been vested to one individual ambapo haiwezekani mtu mmoja afanye maamuzi kwa niaba ya nchi nzima huo ni uendawazimu kutegemea lolote lile.
 
Tumekuwa wapesi kuipinga rasimu ya katiba kumbe Jaji Warioba kayafanyia kazi mapendekezo ya rasimu ya katika yaliopendekezwa na Chadema.

Juzi kupitia hapa JF nilimsoma Dr. Kitilia Mkumbo anasema serikali tatu kuziendesha ni maajabu.

Wananchi hawajuhi washike lipi kwenye hili suala la katiba.
 

nafikiri wanalalamikia zaidi mfumo wa serikali ya shirikisho ndio tatizo kilichotakiwa ni commission ndogo tu kama ya style ya european union kuongoza shirikisho lakini inaonekana kama rasimu imetengeneza seriakli nyingine ambayo ni kama haiitajiki kwani tayari unao mawaziri wa ndani ya serikali zote mbili(bara na visiwani) sasa kuna haja gani tena ya kuwa na mawaziri wengine waziada kwahiyo unaufanya mfumo mzima kuwa very expensive na unnecessary nafikiri hata wazo la serikali mbili la awali la kutokuwa na serikali ya tanganyika lilikuwa lina angukia ktk umuhimu mzima wa kuwepo serikali ya muungano badala ya tanganyika.
 
CHADEMA si wakuhangaika nao mkuu...hawana msimamo hawa.
 
Naona umekunywa gongo na akavuta bangi kabla ya kuja kupost hapa.

Msimamo wa CHADEMA kuhusu serikali tatu uko pale pale na hawajawahi kusema kinyume.
Serikali tatu ni sera rasmi ya CHADEMA.

CHADEMA ni chama makini sana hapa Tanzania, Afrika na duniani kwa ujumla, hawakurupuki katika mambo yao, wamesema kama chama watakaa na kuipitia rasimu yote kisha watatoa msimamo wao kuhusu rasimu hiyo hususani katika mambo ya msingi.

CCM na waliberali tulieni mpate dozi ya moto moto.
 
Wale wote wanapinga serikali tatu hakiwemo Mzee Mwanakijiji, walikuwa wapi kuwapinga Chadema.

well; suala la serikali tatu ni sera ambayo watu wengi wameikubali kwa muda mrefu tangu wakati wa sakata la kina Njelu Kasaka na G55. CUF walikuwa na sera hiyo; CDM walikuwa na sera hiyo na CCM baadhi yao walikuwa na sera hiyo. SEra ya serikali tatu kimsingi ni majibu ya madai ya Zanzibar.

Kwa upande wangu msimamo wangu ni ule kama wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere - kutoka serikali mbili kwenda serikali moja. Huo ni msimamo wangu binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…