Uchaguzi 2020 CHADEMA mjirekebishe kwenye Media Management

Uchaguzi 2020 CHADEMA mjirekebishe kwenye Media Management

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
225
Reaction score
910
Sasa ndugu zangu wa CHADEMA, kama mnajua fika kwamba serikali kupitia Dr. Abbas na TCRA wanahujumu katika vyombo vya habari kwanini msitumie mbinu mbadala kwenye press conference zenu na pia hata mikutano yenu?

Katika presser ya Tundu Lissu leo, chombo kimoja tu - DAR MPYA - ndicho kilikua kina stream live, na kinastahili kupongezwa kwa hilo. Lakini kuna muda kulikua kuna technical difficulties. Kuna muda sauti ilikua haiskii, kuna muda ilikua inakwama, na mwisho kwenye kujibu maswali live stream ikakatika kabisa.

CHADEMA ina channel yake YouTube kwanini isingetumia hiyo channel kulivestream? Au kwanini wasingelivestream kupitia twitter kama wanavyofanyaga?

Vyombo vingi naona vilikuwepo kwenye presser ila tunajua watafilter baadhi ya vitu alivoongelea Lissu. CHADEMA TV iwe source ya watu kwenda kusikiliza wagombea wa chama chao wanongea nini.

Naomba mjirekebishe katika hili.

All the best!
 
Jamani hili ni kweli kabisa. Hapa sijui kwa nini hawapafanyii kazi. Hivi kampeni zikianza itakuwaje? Huku mnajua kabisa hamtapewa airtime huko kwingine, halafu media yenu hamshughulikii. Hapa CHADEMA mparekebishe jamani. Inakera sana.
 
Back
Top Bottom