CHADEMA mkiingia Ikulu, badilisheni jina la TBC kuwa Tanzania TV

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Mwenendo wa TV inayoendeshwa kwa kodi za watanzania wote bila kujali vyama vyao, ni mbaya. Wanaonesha LIVE mikutano ya kampeni za CCM pekee.

Kama walitofautiana na CHADEMA, kwanini hawaoneshi LIVE mikutano ya vyama vingine mfano ADC, CHAUMA, ACT, CUF na vingine? TBC nawachukia kama ninavyochukia POLICE, WAKURUGENZI pamoja na NEC.

Lissu ukiingia Ikulu, badili jina la TBC kuwa Tanzania TV na redio inawezaitwa Radio Tanzania. Fumua idara zote na uanze kumtumbua mkurugenzi wake. Pia fumua jeshi la polisi pamoja na NEC.
 
Hakuna ulazima wa kubadilisha jina! Hapo ni kuwatimua tu makada wote na kuleta damu changa iliyojaa vipaji! na pia kuwarudisha nyumbani mastaa wote muhimu walioko ughaibuni kwa lengo la kuja kuliongezea ufanisi zaidi Shirika letu.
 
Sasa jina lao ndio lililo kutenda hayo? Sio watu!
 
Sawa ila ishu sio redio, wale wanashindwa kutumia taaluma zao kutokana na mfumo ila ni vijana weledi mnoo
 
Unatatizo mahara wewe sio buree
 
Kuanza upya ni jambo jema ili kuondoa ile dhana ya TBCCM
Hakuna ulazima wa kubadilisha jina! Hapo ni kuwatimua tu makada wote na kuleta damu changa iliyojaa vipaji! na pia kuwarudisha nyumbani mastaa wote muhimu walioko ughaibuni kwa lengo la kuja kuliongezea ufanisi zaidi Shirika letu.
 
Hakuna ulazima wa kubadilisha jina! Hapo ni kuwatimua tu makada wote na kuleta damu changa iliyojaa vipaji! na pia kuwarudisha nyumbani mastaa wote muhimu walioko ughaibuni kwa lengo la kuja kuliongezea ufanisi zaidi Shirika ‘
Itasaidia maana hadi mda huu mimi nimeshapata allergy nikisikia tu tbc nachefukwa vibaya mno.
Sasa tubadili jina sababu ya allergy na vichefuchefu vyako mtu mmoja. Si bora tuhangaike kukutibu tu upone!
 
Sasa tubadili jina sababu ya allergy na vichefuchefu vyako mtu mmoja. Si bora tuhangaike kukutibu tu upone!
Mheshimiwa, umejisikia tu kuni quote, au!! Kulikua na ulazima wowote wa kunihusisha na hiyo allergy?
 
Mheshimiwa, umejisikia tu kuni quote, au!! Kulikua na ulazima wowote wa kunihusisha na hiyo allergy? Kama ilikuwa inaelekea kukwaza, basi disregard tusonge mbele.
 
Huko jamhuri ya Twitter itaitwa Ufipa TV.
 
Leo TBC kutwa nzima waliokuwa busy kumnadi JPM kwa kisingizio cha kumpongeza kwa miaka mitano.

Hatuna television ya Taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…