Uchaguzi 2020 CHADEMA mkimsimamisha Lissu najiunga na chama chenu

Mleta Ni like Chadema time la siku nyingi nalijua hili .Mada zake nyingi Ni za kusifia Chadema sio chama kingine kiwe CCM au chochote

Kuna tofauti za wazi katika kusifia mada zenye mashiko na kusifia mada kwa sababu tu ni ya chama fulani.

Hapo ndipo tunapoachana njia panda.

Pasipo na mashiko kuelezana bayana pasi na kuangalia makunyanzi, kutatuokoa sote salama sisi kama taifa.

Ushabiki ushabiki kwao Mbao, Ndanda, Mtibwa au hata Namungo FC.
 
CCM ipi unayoitaja ile Mliyokuwa mnaiita ya Mafisad ambao wote Wapo Chadema ambacho kwasasa kinaitwa Chama cha Kulinda Waharifu (Waliowataja Wenyewe)
 
Mleta Ni like Chadema time la siku nyingi nalijua hili .Mada zake nyingi Ni za kusifia Chadema sio chama kingine kiwe CCM au chochote
Ndio akili za vijana wetu, nakuambia nimejiunga mwaka mmoja tokea CCM izaliwe yaani 1978 tena nikiwa JKT na kulikuwa na hekaheka za vita kule Kagera.
Pengine wewe ulikuwa hujazaliwa bado.
Unashangaa nini kukubali kwangu kumuunga mkono mgombea bora tokea chama kingine kama huyu tulie naye katuharibia chama?
CCM haikupaswa kuwa na propaganda za kitoto kama zilivyo sasa, ukatili kwa RAIA tunao uona ukifanyika, uongo wa kupitiliza hadi kutufanya wanachama tuonekane wajinga mbele ya jamii na kutoheshimu katiba na sheria.
Tanzania ni ya wote, na ninahakika Nyerere angekuwa hai asingekubali ccm iwe ilivyo na angeshindwa angeiacha.
Hata Kikwete kama mlimsikiliza Kyle Lupaso ni kuwa amechoka karibu atamwaga manyanga au kesha mwaga moyoni bali anaogopa akiwa wazi nini hatma yake? Na jee utawala nje ya ccm nao utakuwaje katika kuheshimu ulinzi wa katiba na kumuacha apumzike?
Nadhani Lissu na serikali yake haitaweka visasi, naye ajitokeze tuu kama Mimi na wengine
 
Mleta Ni like Chadema time la siku nyingi nalijua hili .Mada zake nyingi Ni za kusifia Chadema sio chama kingine kiwe CCM au chochote

Sidhani ndugu mkereketwa mwenzangu na mimi wa Lumumba.

Ukweli ni kwamba ndani ya chama kuna watu mioyo inavuja damu.

Ndugu zangu wanaCCM wenzangu tusidanganywe na utitiri wa watia nia udiwani na Ubunge. Ukweli ni kwamba asilimia 90% ya watia ni wasaka tonge, nothing more. Ukijaribu kuchunguza wengi wao mwaka 2015 walihama na Lowassa either physically au kimoyomoyo.

Mimi siondoki CCM nitabaki na kuwa mpinzani hukuhuku, haijalishi wataniita mhujumu na msaliti. Ila tutaambiana ukweli humu humu.

Buku saba sio saizi yangu, mali ya umma ni ya umma hauwezi itumia bila kufuata taratibu rasmi zilizowekwa.

Kauli mbiu kuelekea 28 October ni hii "#Where is 1.5 trillion?"
 
Amina
Haja ya maombi yako itimie!
 
Usiwe na hofu kamanda Lissu anasimama.
 
Nakubali na Lissu is the best option that we have. Fikiria Kenya hawajaja msibani sababu wanajua kilicho muondoa mzee ni COVID 19. Lakini sisi tumekomaa kudanganya umma wakati kifo kinatuumbua
 
Kama ulijiunga CCM mwaka 1978, unakwenda Chadema kutafuta nini? Mbona huko Chadema kwenyewe kuna waongo, wazandiki, wambea waliompakazia Mzee Kinana kwamba anafanya biashara ya meno ya Tembo wakati si kweli? Au unataka kwenda kuwadukua tu halafu urudi CCM?
 
Yaani tumekosa watz wa kuwapa kuongoza nchi mpaka tumpe mlemavu
Mkuu siasa zimekupelekea hadi uandike kitu cha ajabu namna hii?!!
Walemavu siyo watu? Kulemaa mguu kunamzuwia nini kuwa raisi wa nchi?

Haya maisha huja yamaliza bado usijitafutie mabalaa ukapata ulemavu utajutia hii kauli yako.

Lissu mimi simkubali kamwe lakini si kwa sababu ya ulemavu wake.
 
Ndugu yangu, kwa heshima ya mzee mwenzangu Kinana acha nisiseme mengi. Lakini ukae ukijua sio kila kitu kinachoamuliwa mahakamani ndio ukweli wenyewe, wakati mwingine kukosekana Solid evidence kunasababisha maamuzi tenge
 
Vipi huko chadema viongozi wadogo wananemekaje?
 
Mimi mwenyewe niliachana na ushabiki wa vyama baada ya Chadema kumpokea lowasa na kumfanya kuwa mgombea wao huku lisu mwenyewe akiwa mpiga debe namba moja huku akiwatukana waliokuwa wanapinga mchakato uliotumika kumpokea
 
Hakuna wa kumlinganisha na Dr slaa hapo chadema kwa Sasa, alisimamia ukweli aliouamini na misingi ya chama hadi pale wenzake wote walipomsaliti kwasababu ya matumbo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…