CHADEMA mna mpango gani na Dodoma?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Tumeona maandamano katika majiji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Mwanza.

Nia ya maandamano ni kuamsha umma kudai HAKI zao na kushinikiza Serikali kupunguza Kodi Ili kuondoa mfumuko wa bidhaa, Kupata Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote, nk nk

Na mwitikio umeonekana kuwa mzuri,

Swali LANGU ni je, lini CHADEMA itapeleka mwamko huo Dodoma na maneno ya Jirani ambako CCM wanadai ni ngome Yao?

Ni Kweli watu wa huko mfumuko wa Bei za bidhaa na gharama za Maisha hazijawaumiza vya kutosha kuikataa CCM?

Kwa jinsi chama hiki kinavyotesa Watanzania, hakipasi kuwa na ngome yoyote Nchi hii.

Muda haujawahi kutosha.

NB: Tanga na Dodoma ni majiji pia,mwl Nyerere hakuyaacha nyuma katika harakati za Ukombozi, lisisahaulike Hilo.

Karibuni πŸ™
 
Hapo Dodoma hakuna mgao wa umeme?
 
mlikofanya maandamano yaliyodorora na hayakua na tija πŸ’

kwa uchovu ule, kibaraka hawez tena kutamani hiyo jogging ambayo haina maana yoyote zaidi ya kuhatarisha afya yake ambayo inaweza kusababisha mambo mengine πŸ’
 
mlikofanya maandamano yaliyodorora na hayakua na tija πŸ’

kwa uchovu ule, kibaraka hawez tena kutamani hiyo jogging ambayo haina maana yoyote zaidi ya kuhatarisha afya yake ambayo inaweza kusababisha mambo mengine πŸ’
Ulijuaje yamedorora au yamefana bila kuyafuatilia?

Jikite kwenye mada.
 
Ulijuaje yamedorora bila kuyafuatilia?

Jikite kwenye mada.
kwani yalikua yanafanyika mafichoni ndio nisijue πŸ’

mada ipi sasa wakati msingi wa hoja wa hoja yako ume-base maeneo uloyataja...

nami nakueleza kwamba hapakua na tija wala maana yoyote. Jogging ilikua imedorora kwa hiyo hamna haja kuendelea kufanya kitu ambacho hakina tija wala maana yeyote πŸ’

zaidi sana kibaraka hata tamani tena kushiriki hiyo jogging labda iwe ni mita mia2 tu zaidi ya hapo labda atembee akiwa kwenye gari πŸ’
 
Dodoma hakuna machali wa CDM ,wanapaogopa kama UKOMA
 
Usituletee nuksi hapa Capital City yetu, upuuzi wa maandamano peleka huko Kwa wavuta bangi na walalamishi wa Arusha na Mbeya.

Mwanza,Dar na Dom in fact Chadema imekataliwa kitambo japo inalazimisha
 
Huko kwingine ilikwenda bahati mbaya lakini shabaha kubwa ilikuwa ni kanda ya kaskazini kule kinapotoka chama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…