LGE2024 CHADEMA mnasikitisha hamuaminiki tena

LGE2024 CHADEMA mnasikitisha hamuaminiki tena

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam,

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa mwezi ujao naona CHADEMA mmeamua kulamba matapishi yenu kwa kushiriki uchaguzi ambao kwa vyovyote vile hamuwezi kuashinda kwani kwa 90% wazimamizi wote wa uchaguzi ni makada wa CCM.

Inashangaza kwenda kwenye uchaguzi kisha mkishashindwa mtaita media na kulalamika kinafiki kwamba uchaguzi haukua huru na haki na kwamba mmeibiwa kura.

Ilikua ni swala jema mngewaacha ccm na washirika wake kina ACT na CHAUMA wagawane hiyo mitaa mngejenga imani kwa watanzania kuwa kweli nyinyi ni Chama cha Democrasia na maendelea na mchakato wa kudai Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini kitendo cha kushiriki kitu mlichowaminisha watanzania ni haramu ni kubariki hiyo haramu.

My take:
Ukiisha uchaguzi msithubutu kuitisha media na kulalamika mumechezewa rafu huo utakua ni unafiki zaidi ya unafiki.
 
wasalaam.
kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa mwezi ujao naona chadema mmeamua kulamba matapishi yenu kwa kushiriki uchaguzi ambao kwa vyovyote
Hivi huoni kama wakisusia uchaguzi ndiyo watakuwa wamejizika kabisa kwani hawa watashirikisha vyama vyao shikizi vya kwenye briefcase ili ku justify ushenzi wao.
 
Na sisi tule, yaani wwle peke yao miaka mitano tena
 
Chama kisichoshiriki uchaguzi kinafaa kufutwa kwani kitakuwa na agenda nyingine nje ya siasa
 
Hivi huoni kama wakisusia uchaguzi ndiyo watakuwa wamejizika kabisa kwani hawa watashirikisha vyama vyao shikizi vya kwenye briefcase ili ku justify ushenzi wao.
Ni kweli. Lkn vipi kama chadema inahujumiwa waziwazi na kuporwa ushindi?
 
Kazi ya chama cha siasa ni kufanya siasa na uchaguzi ndiyo tukio kubwa la kisiasa, hivyo mbali ya kutafuta ushindi kwenye sanduku la kura lakini pia chama kinapata uwanja mpana wa kuvutia wafuasi wapya.
Kwa sababu hiyo si busara kwa chama cha siasa kususia uchaguzi
 
Baadhi ya viongozi wa chadema top layer wapo kazini mkuu
 
Chama hakiandai viongozi wanategeshea waloshindwa kura ya maoni CCM ndo wapeperushe bendera zao,aibu kabisa. Kwenye kata yangu ya Businde Kyerwa Kagera yenye vijiji 3 wamesimamisha mgombea mmoja tu nafasi ya uenyekiti wa Kijiji, na ambaye alishindwa kura ya maoni ya CCM. Alafu mtu anaongea bila aibu kwamba anaenda ikulu 2025!!?
 
Wasalaam,

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa mwezi ujao naona CHADEMA mmeamua kulamba matapishi yenu kwa kushiriki uchaguzi ambao kwa vyovyote vile hamuwezi kuashinda kwani kwa 90% wazimamizi wote wa uchaguzi ni makada wa CCM.

Inashangaza kwenda kwenye uchaguzi kisha mkishashindwa mtaita media na kulalamika kinafiki kwamba uchaguzi haukua huru na haki na kwamba mmeibiwa kura.

Ilikua ni swala jema mngewaacha ccm na washirika wake kina ACT na CHAUMA wagawane hiyo mitaa mngejenga imani kwa watanzania kuwa kweli nyinyi ni Chama cha Democrasia na maendelea na mchakato wa kudai Tume Huru ya Uchaguzi.

Lakini kitendo cha kushiriki kitu mlichowaminisha watanzania ni haramu ni kubariki hiyo haramu.

My take:
Ukiisha uchaguzi msithubutu kuitisha media na kulalamika mumechezewa rafu huo utakua ni unafiki zaidi ya unafiki.
Subira umeacha kuvuta kheri sasa hivi unavuta Bangi!!
 
Naungana na CHADEMA kushiriki uchaguzi huu.
Wakisusia watajimaliza kisiasa na haitabadili uovu wa wanaochafua uchaguzi.
Washiriki ili watu wenye kupenda haki duniani kote waone ubaya watakaofanyiwa wapinzani endapo kweli watafanyiwa au wanafanyiwa.
 
Back
Top Bottom