Uchaguzi 2020 CHADEMA mnawaangusha sana Watanzania. Hawatawasamehe kamwe!

Uchaguzi 2020 CHADEMA mnawaangusha sana Watanzania. Hawatawasamehe kamwe!

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Amani iwe nanyi wadau,

Kama mnavyojua watanzania, kampeni zimeanza rasmi kwa ajili ya uchaguzi Mkuu. Vyama Vikuu vinavyoshindana mwaka huu kwa Upande wa Tanzania bara ni Chadema na CCM na upande wa Tanzania visiwani ni ACT na CCM.

Ni siku ya pili tangu kampeni zianze rasmi leo naomba niwape ujumbe mgumu Chadema kwa sababu kama chama kinachopendwa na watanzania wengi, wengi tunafikiri kuwa kingekuwa very serious kwenye uchaguzi huu ila tunachoona sasa ni kama hawapo serious tena kwa makusudi.

Nasema haya kwa sababu zifuatazo:

1. Suala la Fedha na Bajeti
Chadema wanasema kuwa hawana fedha za kutosha za kampeni. Jana Mgombea wao alitoa namba kadhaa kwa ajili ya chama kuchangiwa kwenye kampeni. Hivyo kwa watanzania tulitegemea kwenye ulimwengu huu wa social media, pages za viongozi wa Chama pamoja na Chama pia kwenye mitandao yote kusheheni matangazo ya kukichangia chama na kuhamasisha watu watoe chochote kuanzia shs 250 hadi kiwango cha juu wanachoweza. Ila mpaka sasa sijaona popote, kuanzia kwenye page ya Lissu, Mdee, Mnyika, na hadi Chama kwenye posts za namna hii. Sasa kama mnataka kweli fedha za kampeni kwanini hamhamasishi hili? Watu wapo wa kuwachangia ila hawaoni matangazo popote. Humu tu tangazo limeletwa na member tu wala sio kiongozi wa Chama wala account ya Chama!

2. Idara ya Habari ya Chama kulala na kuzubaa
Watanzania wote wanajua kuwa CCM wamejipanga kuwafanyia fitna kwenye media. Media zote haziko na nyie na nyingine zinakata matangazo yetu. Badala ya nyie kuja na njia mbadala ya kutumia Media yetu kufanya live streaming nyie mnalala. Hiki ni kipindi cha kampeni, tulitegemea kutakuwa hata na clips zilizoandaliwa kiustadi zikimwonyesha mgombea wenu akiongelea mipango yake na sera zake endapo atachukua nchi, clip hizo zingesambazwa kwenye social media zote hasa Facebook, Twitter na Instagram ili watu wazione maana kwa sasa watu wengi wapi huko. Ila hata huu ubunifu tu mmeshindwa kuwa nao!

Hata kuhusu mikutani ya chama chenu. Hakuna uhamasishaji, hakuna hata matangazo ya kutosha hasa kwenye social media ambapo watu wengi wapo. Idara ya Habari Chadema hamfanyi kazi yenu vizuri.

3. Team ya Kampeni ya Lissu kutoonekana
Jana tumeona mkutano wenu wa Mbagala. Ndio mlisema hamuwezi kutoa sera as long as Wagombea wenu wametolewa ila Je sasa kama mnashiriki uchaguzi hamkuona kuwa ilitakiwa hata mgusie sera zenu watu wavutiwe na nyie?

Siku zote Chadema kinapendwa na wasomi na watu wanaojielewa. Kundi hili ni kundi la kusikiliza Sera na sio mziki kama CCM. Sasa nyie mnafeli wapi? Lazima siku zote mjitofautishe na Chama cha Mapinduzi. Na tofauti yenu lazima iwe sera nzuri na bora sasa kwa nini mnashindwa hata kwa dk 45 tu kuelezea Sera zenu nzuri na bora!

Mwisho tunajua CCM wanafanya mabaya mwaka huu. Wananchi hawayapendi ila kama nyie Chadema lazima mfanye kazi kwa nguvu kuhamasisha wananchi na sio kuleta mzaha na upuuzi. Mwageni Sera, hamasisheni watu kuja kwenye Mikutano, tengenezeni video clips na documentaries za sera zenu na risheni Twitter, Facebook na Insta watu wataona na kushare na watakuja kuwasililiza kwa wingi.

Naomba niishie hapa!
 
Ukweli kuna pahala Chadema mnakwama. Hasa kwenye kipengele cha kukusanya michango ingawa najua.pia kwa serikali hii kuna ugumu wake. Msije mkapewa case ya ml
 
Inawezekana chadema hawana nia ya kuchukua mamlaka ya kuiongoza nchi ndo mana hawako siriazi kwenye mambo siriazi
 
Umeanza kuona e? Sasa wewe ni mfia chama umeona hilo, wanaweza kukuambia wwe ni kama nani unaongea maneno haya.
 
Ukweli kuna pahala CDM mnakwama. Hasa kwenye kipengele cha kukusanya michango ingawa najua.pia kwa serikali hii kuna ugumu wake. Msije mkapewa case ya ml
Hakunaga michango bila hamasa, wanatakiwa kulijua hili hakika
 
Umeanza kuona e? Sasa wewe ni mfia chama umeona hilo, wanaweza kukuambia wwe ni kama nani unaongea maneno haya.
Kwenye mapambano kuna kukumbushana!!! Watu wasisahau wajibu wao!!!
 
Back
Top Bottom