CHADEMA msijilamu, ninyi ni kimbilio la walioteswa

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
1,382
Reaction score
2,582
Ni kawaida kwa binadamu kutafuta faraja pale anapoumizwa.

Katika vyama vya siasa watu huumizana sana na kuvurugana, wengine hufikia kiasi cha kutishiana maisha. Ikifika hali hiyo wengine hukimbia kwa jirani kutafuta faraja. Wapo ambao huwa hawarudi kabisa, wengine hurudi kama amani ikilejea kule kwao.

Swala hili si la vyama vya siasa tu, hata kwenye nchi, kuna watu hukimbia nchi zao kwa sababu za migogoro ya kisiasa, hali inapotulia nyumbani huamua kurudi wapo wengine wanaomua kuchukua uraia wa huko waliko. Hivyo basi hii ni kawaida kabisa wala msiogope.

Labda jambo la maana, msiwe wepesi wa kuwapa nafasi za uongozi hawa wanaokuja kutafuta faraja. Wapeni muda mrefu wa matazamio.
 
Chadema ni nuru iwamulikayo wahangaikaji ndio maana wote huikimbilia as there first destination, hilo halina ubishi, vyema wakiondoka waweke akiba ya maneno wasije kujuta mbele ya safari.
Hicho kiinglishi umeniacha kidogo bwashee!
 
Uko sahihi kabisa,chadema inazidi kuwa imara na ndicho chama mbadala kwa sasa.Wananchi na wapenzi wanakipenda wenyewe toka moyoni bila shuruti. Wageni si vyema kupewa vyeo vya juu kwa sasa bado tuna hazina kubwa ya vijana wenye weledi kwa sasa tuwape kipaumbele.

Walioondoka baada ya kupata faraja ruksa wala hatuna hiana nao.Bila ushindani wa kisiasa nchi itakwenda kama mkokoteni unaovutwa na punda
 
Hicho kiinglishi umeniacha kidogo bwashee!
🤣🤣Kua muungwana mkuu, kosoa huku unamfundisha, maan yaezekana hajaelewa amekuachaje. Aidha amekuacha kwamba hujui lugha ya malkia au lugha ya malkia aliyotumia haiendani na alichokusudia kusema.
 
🤣🤣Kua muungwana mkuu, kosoa huku unamfundisha, maan yaezekana hajaelewa amekuachaje. Aidha amekuacha kwamba hujui lugha ya malkia au lugha ya malkia aliyotumia haiendani na alichokusudia kusema.
Hahahaaaa...... Pale kwenye " there" ndipo aliponiacha bwashee!
 
Hahahaaaa...... Pale kwenye " there" ndipo aliponiacha bwashee!
Najua 🤣🤣sema hii mambo wakati mwingine ni kupeana elimu na kufundishana, lugha ya malkia unaweza ona rahis kuandika unachotaka kumaanisha but kwenda kweny maana halis inakua tofaut
 
Ni kweli ni chama mbadala lakini hakina budi kubadili mtindo au political strategies. Misimamo isiyoenda na upepo wa kisiasa kwa wakati husika ni janga kwa hiki chama.

Uongozi wa chama hichi unatakiwa kubadili mtazamo wa masuala muhimu ya nchi na kwenda sambamba na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na utamaduni.

Short of that ACT WAZALENDO itachukua nafasi ya chama mbadala muda c mrefu na hii ni kwa sababu kiongozi mkuu wa ACT WAZALENDO ni mwanasiasa mjanja na anayekwenda sambamba na mabadiliko ya upepo wa kisiasa na hali halisi ya mambo!
 
Kiongozi kipofu, na mlevi wa faru John akimwongoza kipofu mwenzake wote hutumbukia shimoni. Mpaka siku akili zikiwajia ndio mtajua, mlikuwa mnakaanga mbuyu.
 
Kwa lugha ya chama tawala wakirudi walikotoka kwa kuwa kumenoga hufaamika kama "ng'ombe waliokatwa mikia"
 
Ni vigumu sana ukijipeleka chadema na kutaka kuwa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…