CHADEMA msitumie CORONA kama moja ya ajenda ya kwenda Ikulu. Someni alama za nyakati. Kwa hoja ya CORONA Magufuli ni Shujaa kwa Watanzania walio wengi

bumilo

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
352
Reaction score
175
Mods naomba msiunganishe Uzi huu ubaki kama ulivyo. Natumaini hamjambo wana JF wenzangu.

Nilirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Ni dhahiri kuwa kutokana na janga lililoikumba dunia na hatua zilizochukuliwa na kila nchi, hapa kwetu Tanzania hatua zilizochukuliwa na Rais wetu zimeonekana kumpandisha chati hata kama kulikuwa na mambo mengine mabaya juu yake. Anaonekana shujaa miongoni mwa Watanzania.

Kila mahali vijiweni na kwingineko ukipita na kuzungumzia suala la CORONA na hatua zilizochukuliwa na serikali wananchi wanapongeza sana na hasa wakiangalia na kusikia masaibu yanayowapata majirani zetu kutokana na mazuio mbalimali yaliyowekwa na serikali zao dhidi ya RAIA wao

Nafikiri kama kweli CHADEMA wana mpango wa kwenda Ikulu nawashauri watafute ajenda nyingine ambazo zinaonesha udhaifu wa serikali iliyoko madarakani la sivyo Ikulu kwao itakuwa ni ndoto

Kumbuka "Wakati ni mwalimu mzuri sana katika maisha ya mwanadamu "
 
Shuja wakati alituma mpaka ndege kwenda Madagascar kuleta dawa ambayo hata haileweki?

Tushukuru tu Africa Mungu katunusuru na sio kusema eti fulani ni shuja katika kupambana na Corona wakati alikuwa hana uhakika.
 
Tushukuru tu Africa Mungu katunusuru na sio kusema eti fulani ni shuja katika kupambana na Corona wakati alikuwa anabahatisha tu.
Tumieni ajenda ya Corona itawapeleka Ikulu na huyo Msaliti Lissu!!
 
Shuja wakati alituma mpaka ndege kwenda Madagascar kuleta dawa ambayo hata haileweki?

Tushukuru tu Africa Mungu katunusuru na sio kusema eti fulani ni shuja katika kupambana na Corona wakati alikuwa anabahatisha tu.
Ndo ujue kuwa Tanzania ni mojawapo ya mataifa pendwa sana na Mungu, ndo maana hekima ambayo Mungu alimpa Mh. raisi ya kutangaza taifa tuingie kwenye maombi ya kufunga na kuomba pamoja na kumshukuru ndo Neema pekee tunayotembelea. Sasa kuna mgombea mmoja amejitoa ufahamu na kusema safari hii hatamwachia Mungu niu......uliopitiliza. Kama Mungu amemuona hawezi, kwa hiyo atamtaka devil?
 
Acheni kulazimisha/kutafuta sifa za kijinga!
 
Huyu ndugu amekosa mtu wa kumshauli hapo ufipa, bora wangempa membe apeperushe bendera
 
Shuja wakati alituma mpaka ndege kwenda Madagascar kuleta dawa ambayo hata haileweki?

Tushukuru tu Africa Mungu katunusuru na sio kusema eti fulani ni shuja katika kupambana na Corona wakati alikuwa hana uhakika.
saa hizi ndio mnakubali kweli corona haipo tz[emoji16][emoji16][emoji16]

nyinyi watu ni zaidi ya matapeli ccm.
 
Acheni kulazimisha/kutafuta sifa za kijinga!
Je, unamuona anaapply social distancing au kuvaa barakoa? Acha upopoma Salary slip, mshaulini ndugu yenu anatoa boko hatari kwenye suala la Korona.
 
saa hizi ndio mnakubali kweli corona haipo tz[emoji16][emoji16][emoji16]

nyinyi watu ni zaidi ya matapeli ccm.
Hizo maiti zinazozagaa mtaani unaziona? Na zile zinazozikwa usiku unaziona?
 
Nadhani hujaelewa hoja ya Lissu! Hoja ya Lissu sio kuwa watu wakae lockdown hakuna sehemu ambayo Lissu amewai sema watu wakae lockdown.

kwenye korona jambo pekee alilofanya Magufuli ni kukataa lockdown na hapo wala hakuna sehemu ambapo Lissu aliwai sema nchi iende lockdown.

Issue ya Lissu ni kuwa magufuli hakujali maisha ya watu hata siku moja tangu Corona ianze. Aliikejeli pamoja na watu kadhaa kufa na hakuonekana kujali maisha ya watu wake.

Hapa Hata mie ninakubaliana na Lissu kwa sababu hakuna sehemu iwe Tweeter au Facebook au kwenye hotuba zake niliwai sikia au nimewai sikia magufuli hata akiwafariji watu waliofariki kwaCorona. Kama ipo hapa mleta mada tuwekee hapa jukwaani tuione.

Mimi mwenyewe nimepoteza marafiki wawili kwa Corona. Mie sivai barakoa lakini sijawai dharau corona au kufanya watu waidharau bila kuchukua tahadhari.

Mwisho niseme nchi nyingi za Africa athali ya Corona haijawa kubwa kama nchi nyingi za Ulaya na America. Hata Congo Maisha yanaendelea, Rwanda vifo ni vichache sana. Kuna nchi Kama Ghana , Nigeria na nyingi za Africa magharibi maisha yanaenda kama kawaida. Kwa hiyo sio Tanzania tu, nchi nyingi za Africa Corona haijawa big issue. Ila hili halimaanishi kuwa wagonjwa na victims hawapo!!!
 
Shuja wakati alituma mpaka ndege kwenda Madagascar kuleta dawa ambayo hata haileweki?

Tushukuru tu Africa Mungu katunusuru na sio kusema eti fulani ni shuja katika kupambana na Corona wakati alikuwa hana uhakika.
Wewe Ni mjinga "eti tushukuru tu Afrika Mungu katunusuru"
Kwahiyo unataka kutuaminisha nchi Kama Kenya ambapo watu wanapika Hadi mawe sababu ya lockdown haipo Afrika?
South Afrika je, hayo maambukizi zaidi ya 1millions yametokea Afrika ipi? Hivyo vifo zaidi 700k vimetokea Afrika ipi?

NOTE; SIASA za Maji taka zisiwafanye mpoteze Akili zenu za kung'amua Mambo nakuwa wajinga wajinga tu.
 
Mods naomba msiunganishe Uzi huu ubaki kama ulivyo. Natumaini hamjambo wana JF wenzangu.

Nilirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Ni dhahiri kuwa kutokana na janga lililoikumba dunia na hatua zilizochukuliwa na kila nchi, hapa kwetu Tanzania hatua zilizochukuliwa na Rais wetu zimeonekana kumpandisha chati hata kama kulikuwa na mambo mengine mabaya juu yake. Anaonekana shujaa miongoni mwa Watanzania.

Kila mahali vijiweni na kwingineko ukipita na kuzungumzia suala la CORONA na hatua zilizochukuliwa na serikali wananchi wanapongeza sana na hasa wakiangalia na kusikia masaibu yanayowapata majirani zetu kutokana na mazuio mbalimali yaliyowekwa na serikali zao dhidi ya RAIA wao

Nafikiri kama kweli CHADEMA wana mpango wa kwenda Ikulu nawashauri watafute ajenda nyingine ambazo zinaonesha udhaifu wa serikali iliyoko madarakani la sivyo Ikulu kwao itakuwa ni ndoto

Kumbuka "Wakati ni mwalimu mzuri sana katika maisha ya mwanadamu "

Mwaka huu maji mtaita "mma!"

Hivi kwani wewe ni nani unayetaka kumpangia agenda Lissu?

Au yale yale ya kuchachandua cha kusema from nowhere?

Mtaweweseka sana mwaka huu.

Sina hakika pia unapoandika kuhusu Corona kama unajua kuna watanzania wenzio ambao ni waathirika wa moja kwa moja wa ugonjwa huu au kwako ni mkuki kwa nguruwe tu?

Ni uungwana kuwa makini na hasa kutambua hisia za watu waliopoteza wapendwa wao ili kujichunga na uwezekano wa kuonekana uko katika kuwacheza shere tu.

Uungwana ni matendo.
 
Tundu Lissu hasiingie kwenye mtego wa kuongelea Corona mbele ya watanzania
 
Mods naomba msiunganishe Uzi huu ubaki kama ulivyo. Natumaini hamjambo wana JF wenzangu.

Nilirudi kwenye hoja yangu ya msingi. Ni dhahiri kuwa kutokana na janga lililoikumba dunia na hatua zilizochukuliwa na kila nchi, hapa kwetu Tanzania hatua zilizochukuliwa na Rais wetu zimeonekana kumpandisha chati hata kama kulikuwa na mambo mengine mabaya juu yake. Anaonekana shujaa miongoni mwa Watanzania.

Kila mahali vijiweni na kwingineko ukipita na kuzungumzia suala la CORONA na hatua zilizochukuliwa na serikali wananchi wanapongeza sana na hasa wakiangalia na kusikia masaibu yanayowapata majirani zetu kutokana na mazuio mbalimali yaliyowekwa na serikali zao dhidi ya RAIA wao

Nafikiri kama kweli CHADEMA wana mpango wa kwenda Ikulu nawashauri watafute ajenda nyingine ambazo zinaonesha udhaifu wa serikali iliyoko madarakani la sivyo Ikulu kwao itakuwa ni ndoto

Kumbuka "Wakati ni mwalimu mzuri sana katika maisha ya mwanadamu "
shujaa gani mwoga kiasi hicho aliyekimbia magogoni na kujificha kijijini kwao
 
Back
Top Bottom