Pre GE2025 CHADEMA mtashiriki uchaguzi kwa tume Ile Ile?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
1. Nitashangaa ikiwa CHADEMA itashiriki Kwenye uchaguzi Mkuu 2025 kwa tume Ile Ile wanayoipinga.
NB: Kwann msitafute shughuli nyingine?
Japo mimi sio Chadema ila Chadema itashiriki kikamilifu chaguzi zote kwasababu Chadema walitishia hawatashiriki Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi, hivyo sasa Tume ya Uchaguzi sio ile ile NEC, Tume ya Uchaguzi sasa imebadilishwa jina inaitwa ni Tume Huru ya Uchaguzi.
P
 
1. Nitashangaa ikiwa CHADEMA itashiriki Kwenye uchaguzi Mkuu 2025 kwa tume Ile Ile wanayoipinga.

2. Mkishinda (kiti kimoja cha ubunge wa Jimbo) mnaanza drama tena. Miaka mitano inapita kwa maandamano. Ila Mwenyekiti Yule Yule.

NB: Kwann msitafute shughuli nyingine?
Lengo la mada yako linafahamika.

Sasa ngoja nikufahamishe ujinga wenu upo wapi:

CHADEMA bila kujali ni nani yupo kwenye tume hiyo ni muhimu washiriki uchaguzi ujao kikamilifu kabisa.

Tena wasikose kuweka mgombea katika nafasi yoyote ile nchini; pasiwepo mtu yeyote wa CCM kupita bila kupingwa.

Wanachotakiwa kufanya kuanzia sasa ni kuwahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi wao kabisa kupiga kura. Kila anayeweza kufika kituoni aende akapige kura.
Hilo moja la mhimu sana CHADEMA walitimize toka sasa hadi wakati wa uchaguzi.

Pili. Ni muhimu sana CHADEMA iwape elimu wananchi tokea sasa hadi wakati wa uchaguzi, kuhakikisha kwamba kura zao, walizo piga, hakuna mjinga/mpumbavu yeyote atakaye chezea hizo kura; hata hao watu wa Tume ya CCM, waelewe, wakifanya upumbavu na kura za wananchi wamekwisha habari yao.

Haya sasa, nenda kawaambie CCM wenzio kwamba hata hiyo Tume yao safari hii haiwezi kufanya uchafu wowote.

Umeelewa?
 
Watu mmekosa vya kushangaa ko unataka kwa kuwa ccm hawataki katiba mpya kwa ajili ya manufaa yao na Chadema waingie mkenge wa kususia uchaguzi ila hao ccm wapate mseleleko wa kupata uongozi wa kisiasa bure!
 
Japo mimi sio Chadema ila Chadema itashiriki kikamilifu chaguzi zote kwasababu Tume ya Uchaguzi sasa sio Tume ile ile, Tume ya Uchaguzi sasa ni Tume Huru ya Uchaguzi.
P
Tume ya uchaguzi sasa ni KIRAKA KIPYA KWENYE VAZI KUUKUU, ......DIVAI MPYA KWENYE KIRIBA CHA ZAMANI

Kukiwa na free and fair election,kwa tume yoyote no matter inaitwaje kwa sasa, inaamua ku reflect will of the people, CCM inaanguka MISA YA kwanza tu, Kwenye Ubunge na Urais.
Kwa sasa JESHI la wanainchi linaweza kusimamia haki likiamua.

All in all Mama haitoshi, CCM 2025 lazima isimamishe mgombea Mwingine.

Huyu Mama atamaliza kuuza vitu vyote vya bara.

Watoto na wajukuu watapiga viboko makaburi kwa Ujinga walioufanya vizazi vilivyotangulia kushindwa kuzuia yafuatayo.

1.kuuzwa kwa bandari zetu Bara kwa njia ya MNADA ambao Bunge lilikuwa DALALI.

2.Kuuzwa kwa mbuga za wanyama.

3,Kuuzwa kwa uwanja wa ndege KIA.

NB: kumpa Kugombea ni kufanya jaribio la kijinga la KUMPA BARAKA ZA KUUZA MALI ZA BARA ZILIZOBAKI.

Shime WATANGANYIKA tuamke, Tanganyika kwanza vyama baadae.
🤔🤔🤔
 
Ngoja tuone yatakayojiri uchaguzi sio mbali japo sioni kama watu watakuwa na mwamko wa kupiga kura uchaguzi huu
Hata huko kwenye kujiandikisha kupiga kura hakuna mwamko mkubwa kama zamani. Watakachofanya wakati wa uchaguzi ni kuruhusu wapiga kura kutumia kitambulisho chochote rasmi hata kama sio cha kura. Mfano NIDA, passport, driving licence nk.
 
Lengo la mada yako linafahamika.

Sasa ngoja nikufahamishe ujinga wenu upo wapi:

CHADEMA bila kujali ni nani yupo kwenye tume hiyo ni muhimu washiriki uchaguzi ujao kikamilifu kabisa.

Tena wasikose kuweka mgombea katika nafasi yoyote ile nchini; pasiwepo mtu yeyote wa CCM kupita bila kupingwa.

Wanachotakiwa kufanya kuanzia sasa ni kuwahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi wao kabisa kupiga kura. Kila anayeweza kufika kituoni aende akapige kura.
Hilo moja la mhimu sana CHADEMA walitimize toka sasa hadi wakati wa uchaguzi.

Pili. Ni muhimu sana CHADEMA iwape elimu wananchi tokea sasa hadi wakati wa uchaguzi, kuhakikisha kwamba kura zao, walizo piga, hakuna mjinga/mpumbavu yeyote atakaye chezea hizo kura; hata hao watu wa Tume ya CCM, waelewe, wakifanya upumbavu na kura za wananchi wamekwisha habari yao.

Haya sasa, nenda kawaambie CCM wenzio kwamba hata hiyo Tume yao safari hii haiwezi kufanya uchafu wowote.

Umeelewa?
Nafikiri nivyema wasikose kupiga kura kwasababu hakuna ushindi hata ukiwa mdogo utapatikana kwa kugoma . Hata wale wabunge wengi aliowahi kupata Mh.Mbowe, tume na katiba vilikuwa ni vile vyazamani. Lazima waingize washindani uwanjani ili mechi inoge.
 
Hapana.
Naona hujanielewa ninacholenga.

CHADEMA kuingia kwenye uchaguzi wowote hata chini ya mazingira ya hovyo si kutafuta huo ushindi wa viti vichache vya kugawiwa na CCM.
CHADEMA kushiriki uchaguzi wowote chini ya mazingira ya aina yoyote ni kutafuta ushindi wa halali.
Kuhakikisha kwamba kura zao zote halali walizo pigiwa na wananchi zinahesabika, na hazichezewi na mjinga yeyote yule; awe polisi, au hao tume feki ya uchaguzi.

Ndiyo maana tunahimiza CHADEMA wawaelimishe wananchi umuhimu wa kulinda kura zao. Ni wananchi pekee wenye uwezo wa kufanya hivyo; siyo CCM, siyo polisi, siyo jeshi siyo tume feki ya uchaguzi.
Umenielewa sasa?
 
1. Nitashangaa ikiwa CHADEMA itashiriki Kwenye uchaguzi Mkuu 2025 kwa tume Ile Ile wanayoipinga.

2. Mkishinda (kiti kimoja cha ubunge wa Jimbo) mnaanza drama tena. Miaka mitano inapita kwa maandamano. Ila Mwenyekiti Yule Yule.

NB: Kwann msitafute shughuli nyingine?
Fisi hasusiwi bucha
 
Back
Top Bottom