Chadema mtasusia uchaguzi au mtashiriki kwa katiba hii inayowaangusha kila chaguzi

Chadema mtasusia uchaguzi au mtashiriki kwa katiba hii inayowaangusha kila chaguzi

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Kila kiongozi,mwanachama,shabiki na hata wanaotaka kuingia chadema huja na kiki ya katiba,
akiulizwa swali vipi kuhusu kuitoa ccm madarakani jibu huwa rahisi tu aah tatizo ni katiba tu kama itabadilishwa na kupata tume huru ccm itang'oka.

Hata nyalandu kabla ya kuondoka ccm alianza kuwashwa na katiba
akaja na porojo za kutaka kuwasilisha hoja yake binafsi bungeni kuhusu katiba mpya,

Swali je ndugu zetu safari hamtashiriki uchaguzi kwa kua katiba haijabadilishwa

viongozi mbali mbali serikalini wameshasema katiba si kipaumbele chao priority ni kuwaletea wananchi maendeleo na kufufua uchumi wa nchi

Katiba iliopo kama yalivyo malalamiko yenu kua inaipa nafasi zaidi ccm kushinda

Au mtashiriki kwa kua mnajua kila chaguzi mnashindwa kihalili ila tu viongozi wanazuga kuwa wameibiwa!

Katiba ni ile ile tume ni ile ile!

Safari hii hawapumui na wakipumua wanapumulia magerezani!
 
Back
Top Bottom