Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Salamu kwenu wanaCHADEMA
Nakupeni pole na kuwapa pole wabongo wenzangu kwa matendo ya utekwaji na mauaji ya wananchi wasio na hatia. Kwa kweli nchiyetu kwa sasa hali inatisha, ombea usiingie katika mikono ya hawa chinjachinja, wauaji ambao mikono yao imeloa damu.
Niwapeni pongezi kwa jitihada zenu za kuuonyesha umma na ulimwengu kuwa bongo kuna kuna vitendo vya kuuwawa watu na kuwatupa maporini.
1. Wamezuia maandamano, lakini wamewasaidieni kusambaza ujumbe wa ukatili wao dunia nzima
Ni kweli walisambaza maaskari jiji zima, wakiwa wamebeba silaha za moto, yote ni kutisha raia. Yaani muonekano wa jiji siku ya tarehe 23 ilikuwa utadhani kuna mapinduzi ya kijeshi hivi na "JUNTA" imeteka jiji na askari wao wamekaa kila kona ya jiji. Ilikuwa ni vitisho. Kiufupi ni picha iliyoonyesha udhaifu wa serikali inayodhani ina ridhaa ya watu, lakini inasambaza majeshi mitaani kutisha, kuogopesha raia eti wasiandamane, kitu ambacho ni cha kawaida katika nchi za demokrasia. Serikali dhaifu hujiegemeza kwa majeshi hata kwa mambo ya kuwajibika yanayohitaji kutekelezwa na viongozi wa kisiasa
2. Andaeni maandamano tena na tena mpaka yafanikiwe, Onyesheni peoples power kurudisha political detterance yenu.
Ndugu wanachadema, peoples power siyo lazima kulazimisha EVENT MOJA, bali ni kuwa RESILIENT (VING'ANGANIZI) mpaka jambo lenu litokee na lifanikiwe. Hawa wanaotegemea majeshi huwa wanajiandaa kwa TUKIO moja kulidhibiti, hawana uwezo wa kuzuia PROCESS inayojirudia kwa msisitizo.
Hawana resources za kukusanya askari kutoka nchi nzima na kuwarundika sehemu moja kila siku, kila wiki, kila mwezi. Na certainly hawana resources za kuzuia maandamano sehemu nyinginyingi kwa wakati mmoja. Kumbukeni, mkiacha kufanya maandamano mnatuma ujumbe wa unyonge, dharau na kejeli zitakazoathiri chama chenu zaidi kisiasa, na mnafungulia milango ya makada wenu kutekwa na kufanywa chochote.
Hebu kuweni ving'ang'anizi kama maji, yakiamua kupita hata kwenye mwamba yatahakikisha yanachimba na kuchimba mpaka njia ipatikane. Mkisitisha azma yenu ya kufanikisha hili jambo, basi mtakuwa mmepoteza "detterance ya kisiasa kwa kiwango kikubwa sana
3. Viongozi wa CHADEMA msiogope kukamatwa, kukamatwa kwenu ni tunu ya kisiasa kwenu na ni aibu kwao
Viongozi wa CHADEMA kama kuna zawadi ya kisiasa kwenu na kwa chama chenu ni kukamatwakamatwa na polisi. Kwanza inawaonyesha wananchi namna watesi wenu walivyo muflisi kisiasa, inajenga awareness na inyerest ya umma kujua kinachojiri na mnachopigania, dunia nzima inajua aina ya watawala tulio nao.
Kwa hiyo ni muhimu kuandaa maandamano mengine mengi kwa kujirudia rudia. Watesi hawawezi kupeleka askari kila mahali kila siku. Na hata wakifanya hivyo wanajichoresha. Na kadri wanavyojihoresha ndivyo grip yao ya mamlaka inavyolegea. Kwa hiyo viongozi wa CHADEMA hasa wakuu, msiwe "wazee wa BUSARA" bali wasumbueni hawa watesi mpaka waje na political agenda yenye mashiko, la sivyo watawapigesheni marktime sana.
4. Watesi wenu wako interested kusave face, ila wanajua wazi umma hauwataki
Hii strategy yao yote ya kupeleka majeshi mabarabarani na kuwatisha wananchi yote inalenga "kusave face" yaani kujionyesha kuwa wao wana nguvu, kwao hiyo ni faraja.Lakini wanajua wazi kuwa wananchi hawawakubali.
Wanatumia njia hii ya kuzima maandamano kijeshi ili kutuma meseji kuwa umma hauna interest na ajenda zenu. Wanajidanganya. Wanajua toka walivyopigwa kwenye uchaguzi wa 2015, ikawapelekea kuiba na kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 basi kitu pekee wanachobank on ni kutisha watu ili wakirudia kufanya yaleyale ya 2020 katika uchaguzi mkuu ujao basi wawe wameshauandaa umma kwa kuutia hofu kubwa ili uje kuogopa kufanya uprising kupitia ukatili unaofanywa systematic kuelekea ktk uchaguzi huo.
5. Msiishie kuandaa maandamano tu, ni muda muafaka kuanza kufundisha watu wenu civil disobedience
Hawa maaskari wanaopelekwa njiani kuwatisha watu wanalipwa mishahara kwa kodi zenu hizohizo, nendeni mkajifunze civil disobedience za naming and shaming, kajifunzeni namna ya kutumia mitandao kuwakera watesi. Watesi wenu kama kuna kitu wanakiogopa basi ni taswira ya heshima zao ambazo ni feki kuvurugwavurugwa, nendeni mkachimbue makorokocho yao ya hovyo myamwage wazi watu waone.
Tafuteni njia za kuwacheleweshea au kuwapunguzia au kuwanyima watesi wenu pesa wanazohitaji ili kuendesha maisha ya anasa kwa kisingizio cha pesa za kuendesha nchi. Kwa mfano mkiweka mgomo wa kunywa pombe kila siku fulani, hamtakufa, Mkitangaza kupunguza kuendesha magari yenu, mtawanyima watesi wenu pesa wanayoipata ktk mafuta. Kiufupi mkitarget kupunguza matumizi katika bidhaa zinazowaingizia pesa japo mara moja au mbili kwa mwezi athari yake itaonekana na lazima watesi watafeel pressure itakayowalzaimisha kukaa mezani kwa dhati
6. Mwisho, msiache kuzungumzia mauaji na utekwaji.
Hili ni doa kwa watesi wenu, Endeleeni kupiga kelele ili watu wawaogope hawa watesi, wajitenge nao, hivyo basi kelele zenu huenda zikasaidia waliobaki wasitekewe na kuuawa.
Soma Pia: