Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
JUMA lililopita nilipigiwa simu nyingi sana na wasomaji wa safu hii, hoja kubwa ikiwa walihitaji kupata maoni yangu kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya CHADEMA kufikia David Kafulila na Danda Juju, kuvuliwa nyadhifa zao za uofisa wa makao makuu ya CHADEMA.
Ndiyo maana nikaona nichukue nafasi hii japo kidogo kujaribu kuchangia kwa faida ya Watanzania wengi vijana na wazee ambao wanaonekana kuguswa sana na siasa za CHADEMA.
Kinachofanya Watanzania wengi kuguswa sana na mwenendo wa mambo ndani ya CHADEMA kama ilivyo kwa CUF nimekielezea kwa kina sana huko nyuma tena mara nyingine nikirejea maandishi ya waandishi wengine kama Edward Kinabo, Charles Mullinda (mhariri wangu wa makala) na hata Mhariri wangu Mtendaji ndugu Absalom Kibanda.
Hivyo ni vema nichangie japo kidogo ili wale wanaopenda kusikia mtazamo wangu kuhusu hili wapate nafasi ya kunisikia na kuchambua maoni yangu kuhusu sakata hili ambalo kwa bahati mbaya baadhi wameliita mgogoro ndani ya CHADEMA.
Kwanza kabisa nikiri kwamba Kafulila ni rafiki yangu wa siku nyingi hususan kwa sababu amekuwa mchambuzi wa mambo ya siasa kwa muda mrefu akiwa ameandika makala muda mrefu kabla yangu, lakini pia ni kijana ambaye kwa muda mrefu nimemwona kama mwenye mtazamo unaofanana nami. Anapozungumzia juu ya kujenga upinzani wenye nguvu anagusa jambo ambalo wanaharakati wengi wa mageuzi tunaliimba kila siku na sisi wa Tanzania Daima tumeliimba kwa muda mrefu tukiongozwa na jemedari wetu, Mhariri Mtendaji, Absalom Kibanda.
Tunafanya hivi si kwa sababu Tanzania Daima ni gazeti la chama fulani cha upinzani ama ni la vyama vya upinzani, la hasha! Ni kwa sababu tunazijua faida za nchi hii kuwa na upinzani wenye nguvu mithili ya ule uliopo nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, na kwingineko ambako chama fulani hakina hatimiliki ya kuiongoza nchi na hivyo hufanya kila jambo kwa tahadhari kubwa na muhimu zaidi kwa kuangalia masilahi ya watu wao kwa kuwa kuteleza hata kidogo tu na kujifanyia mambo ya binafsi au mambo ambayo ni kwa maslahi ya chama chao kama tunavyoona hapa nchini kwetu, itakuwa ni tiketi ya wao kuondolewa madarakani.
Katika hilo tumekuwa pamoja na Kafulila kwa kipindi kirefu. Na ndiyo maana amekuwa huru sana kunieleza mambo mengi mara kwa mara yanayoendelea ndani ya CHADEMA na mara zote nimekuwa nikitumia upeo wangu mdogo wa kuelewa ambao nimejaliwa na Mwenyezi Mungu kubaini yepi ni halisi yapo CHADEMA, yepi ni imani potofu ya Kafulila, yepi ni hofu tu ndani ya Kafulila mwenyewe, yepi amejikuta akiyatamka kwa sababu ya kutojua na yepi anayaongea kwa makusudi kwa sababu zake binafsi.
Wakati wa mchakato wa uchaguzi wa CHADEMA tuliwasiliana sana na Kafulila kwa kupigiana simu na kutumiana sms, baada ya uchaguzi ule tumeendelea kuwasiliana naye mara nyingi tu, wakati wa kuvuliwa uofisa pia tumeongea sana na baada ya kutangaza kujitoa CHADEMA nilimpigia simu tukaongea naye zaidi ya dakika 18, na siku hiyo alinitaarifu kwamba angejiunga NCCR Mageuzi. Mimi pia ni miongoni (kama kuna wengine) wa watu waliotumiwa ujumbe mfupi wa simu na Kafulila akinieleza comment ambayo alikuwa ameitoa kwa vyombo vya habari kuhusiana na kitendo cha katibu mkuu wa CHADEMA kutengua uteuzi wake kama Ofisa Habari na Uenezi wa CHADEMA. Na hatimaye nimesoma statement yake kwa vyombo vya habari wakati akizungumzia suala la yeye kuondolewa kwenye nafasi yake na azima yake ya kujitoa CHADEMA.
Na mwisho nimesoma kile alichokiandika akiwa anachangia kwenye mtandao wa WANABIDII kuhusu kitendo cha yeye kujitoa CHADEMA.
Naweza kusema sasa bila kuumauma maneno kwamba Kafulila ameshindwa kubadili mwenendo wake ili kuwa compatible (mtanisaidia Kiswahili chake) na wenzake.
Nadiriki kusema hapa kwamba binafsi nilishiriki kumshauri Kafulila kuachana na siasa zake alizokuwa akiziendesha ndani ya CHADEMA na naamini wapo wengine hususan ndani ya chama chake hicho cha zamani waliomshauri pia. Lakini kwa sababu hakusikia yakamfika yaliyomfika. Na mara moja akatangaza kukihama chama.
Napenda niwaeleze tu wasomaji kwamba hoja nyingi alizozitumia Kafulila ni za kale mno na ambazo zimepitwa na wakati na zile zile ambazo wakati fulani akiwa vizuri ndani ya CHADEMA alishiriki kuzitetea.
Ni hoja zile zile za ukabila, viti maalumu vya ubunge, matumizi mabaya ya ruzuku, ubaya wa Mbowe, nk. Ni hizo hizo.
Mambo mengine yanayozuka hivi sasa ya vikao vya siri vya kummaliza Zitto kisiasa na kuwavua uanachama wote waliomuunga mkono Zitto wakati wa uchaguzi mkuu wa chama, Mbowe kuita wahariri watano wa magazeti ili kuwatumia kummaliza Zitto na hatimaye mmoja akakataa, Mbowe kufuja sh milioni 35 za chama, na mengineyo mengi ni kusaidia tu kukoleza hoja hizo hapo juu. Lakini soma kwa mfano nukuu hii hapa chini:
Wakizungumza na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho, Kinondoni, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Erasto Tumbo, alisema taasisi hiyo inayojishughulisha na masuala ya utawala bora inapotosha umma kwa kudai kuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, amechota sh milioni 100 za chama hicho. Alisema kauli ya Ngawaiya si ya kweli na kwamba fedha hizo zilikuwa ni deni ambalo Ndesamburo alikikopesha chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Ngawaia anatakiwa kufahamu fedha hizo ni za Ndesamburo ambaye ndiye alikopesha chama, ili kufanikisha uchaguzi mwaka 2005 na tayari katika kipindi cha miaka mitatu tumekamilisha kurudisha fedha hizo, kwa hiyo Ngawaia hana hoja labda ana chuki zake za kisiasa ambazo anatumiwa na CCM, alisema Tumbo.
Tanzania Daima, Jumanne Januari 20, 2009. Ukisoma habari hiyo utagundua Kafulila alikuwa pamoja na Mkurugenzi wake Erasto Tumbo. Lakini leo anatangaza kitu hicho hicho alichokipinga kwa Ngawaiya yeye akijielekeza kwa Mbowe wakati Ngawaiya alikuwa kwa Ndesamburo.
Ni Kafulila ambaye amekuwa akiisifia CHADEMA, mfano kwenye Tanzania Daima Jumatano ya Juni 13, 2007 Mwanaidi anasema: David Kafulila, mwandishi hodari hupenda kusema: CCM works with a clock while CHADEMA works with a compass. Yaani CCM inafanya kazi kwa kutumia saa wakati CHADEMA inafanya kazi kwa kutumia dira. Maneno haya hawezi kuyatamka leo baada ya kuvuliwa wadhifa wake lakini ameyahubiri sana akiwa mstari wa mbele wa CHADEMA.
Ndiyo maana naiona hatua ya kufutwa kwa Kafulila wadhifa wake na hatimaye kuamua kukikimbia chama kama hatua isiyo na shida yoyote hasa kwa upande wa chama.
Ni kama mtu aliyeshindwa kubadilika tu ili kufikia kwenye mstari unaomkutanisha na wenzake akaamua kutimua mbio.
Lakini CHADEMA kitabaki kuwa chama makini kama kilivyo na kwa kweli binafsi napenda niseme, hivyo kilivyo CHADEMA ndivyo kinavyopaswa kuwa. Mwendo mdundo CHADEMA, chama cha siasa kinahitaji kuwa makini na hakihitajiki kuogopa kuchukua hatua pale inapobidi hata ikibidi kumvua wadhifa wake makamu mwenyekiti au hata mwenyekiti wa taifa, achilia mbali ofisa wa kawaida makao makuu.
Wale waliokuwa wakiniuliza sana kwamba mbona chama kinaingia katika mgogoro itakuwaje? Jibu analitoa Kafulila mwenyewe kwenye makala yake ya Februari 12, 2006 pale aliposema:
Tunaelewa janja ya Bagenda ilikuwa nini? Bagenda alikuwa na agenda ya kuupotosha umma wa Watanzania kuwa vyama vya upinzani na hususan CUF na CHADEMA ni vyama hovyo hovyo.
Kitu ambacho si kweli! Lakini hatuwezi kumshangaa Bagenda kwani anayo yafanya Bagenda ndiyo yaliyofanywa na karibu wasomi wote kila walipotaka kuhama upinzani.
Haya ndiyo aliyafanya Nsanzugwanko, Wasira na sasa - Ngawaiya, ni gia ya kurejea kundini.
Ingawa Kafulila hakuelekea CCM lakini bado maneno yake mwenyewe dhidi ya Bagenda yaweza kuwa maneno yangu dhidi yake.
Nani ajuaye, yawezekana kabisa kwamba kuingia CCM kwa Bagenda kwa mujibu wa Kafulila ilikuwa ni kurejea kundini na kuingia NCCR kwa Kafulila kwa mujibu wa mtu mwingine ikawa ni kurejea kundini, maana kwa maneno yake mwenyewe amenitamkia kwamba ndani ya jimbo lake NCCR ina nguvu kushinda CHADEMA.
Muhimu kwa wana - CHADEMA na wanaharakati wanaoiunga mkono CHADEMA na kuitazama kama mbadala tunaoutafuta, ni kwamba Kafulila mwenyewe anasimama kukanusha akisema si kweli kwamba CHADEMA na CUF ni vyama vya hovyo hovyo tofauti na anavyotaka umma uamini sasa, baada ya kuamua kujitoa na kuingia NCCR. Pengine niwapongeze tu viongozi wakuu wa CHADEMA kwa busara ambayo wamekuwa nayo tangu kuanzishwa kwa chama.
Busara ya kutojibishana hovyo hovyo kwenye vyombo vya habari. Hata katika hili muda mwingi wametulia.
Ni mara chache sana ilipomlazimu Katibu Mkuu kutoa ufafanuzi kwenye vyombo vya habari. Hiyo ndiyo hulka inayotakiwa na hakika chama kitaendelea kuwa imara na pengine kuimarika zaidi bila Kabourou, bila Kafulila, bila Kyara, bila Akwilombe, na bila kiongozi yeyote wa CHADEMA ambaye ana mpango kama wa Kafulila bila kujali cheo ama wadhifa wake ndani ya CHADEMA ama umaarufu wake ndani ya nchi.
Mabadiliko hayatakuja kwa askari laki moja waliojiunga na jeshi wakiwa wamejaa ubinafsi na kujiona kama wao ni wataalamu wa vita kuliko wengine. Mabadiliko halisi yataletwa na askari wachache waliojitoa wakaacha ubinafsi, kujisifu na kujiona wataalamu zaidi badala yake wakawa kitu kimoja katika kusikiliza sauti ya kamanda wa kikosi na kwa pamoja kusonga mbele kumkabili adui.
Rejea makala yangu: Idadi si kikwazo katika kupigania haki. Tanzania Daima, Jumatano Aprili 9, 2008. Tuwasiliane kwa muda kupitia 0719 795 222 baada ya simu yangu kukwapuliwa na kibaka aliyeahidiwa na JK mwaka 2005 kwamba atapewa moja kati ya ajira milioni moja alizokuwa azitengeneze. Baada ya kuzikosa kajiajiri kuwakwapulia simu wale wanaomtetea, na si ajabu mwakani akamchagua tena aliyemwahidi ajira hewa na akikosa baada ya 2010 atapandisha ajira yake mwenyewe na kuwa mporaji wa kutumia sime na silaha nyingine ndogo ndogo.