CHADEMA na ACT msione aibu kutomiliki majengo ya Ofisi

CHADEMA na ACT msione aibu kutomiliki majengo ya Ofisi

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika kipindi cha Medani za Siasa kilichorushwa hivi karibuni Star TV nilishuhudia Ado Shaibu, Katibu mkuu wa ACT akijibu swali la umilikaji wa Ofisi zao kijanja na kwa kona kona nyingi sana kutoka kwa mtangazaji Odemba. CHADEMA nao wamekuwa wakikejiliwa sana kuhusu kutomiliki jengo la Ofisi kubwa kwa muda mrefu.

Ni vyema raia wa Tanzania wenye upto mdogo wakaeleshwa vizuri kumiliki majengo ya ofisi sio kipimo cha uimara wa chama. Kenya ambako kuna ushindani mkali wa kisiasa Chama cha Jubilee cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta na UDA cha Rais wa sasa, William Ruto vyote vimepanga makao makuu yake katika majengo ya watu na wala havimiliki majengo yake binafsi.

Pia chama cha ODM cha Raila Odinga kiongozi upinzani wa muda mrefu mwaka juzi ndio walijenga ofisi yao ndogo tu kama hiyo ya Ufipa. Kumiliki au kutomilikia ofisi kwa chama hakupaswi kuwa hoja katika siasa makini za masuala mazito ya nchi.
 
Shida inakuja viongozi wengi wa hivyo vyama vya upinzani wana mijengo yao binafsi ya maana.

Wataalam wa writeup wanao na wazungu wana mafungu kabisa ya kuboost hizi project wanashindwa vipi kuwa na head office za kisiasa?

Hii siyo excuse.
 
Kwa huko Kenya mazingira ni tofauti, lakini kwa hapa nchini, CDM hawakupaswa kukosa ofisi yenye hadhi ya chama hicho. Kuna ya kutetea lakini sio hili boss.
 
Back
Top Bottom