Uchaguzi 2020 CHADEMA na ACT Wazalendo andaeni mdahalo kati ya Tundu Lissu na Bernard Membe tuwapime!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kuelekea ushirikiano wa kusimamisha mgombea mmoja wa upinzani napendekeza pawepo na mdahalo wa wagombea ili wapiga kura tuwstathmini.

Wagombea wakuu Tundu Lissu na Bernard Membe na ikiwezekana ashirikishwe na mzee Hashimu Rungwe Spunda.

Hii itasaidia kuwaelewa wagombea wetu na kuimarisha mshikamano pale mmoja wao atakaposimama kuwakilisha upinzani.

Maendeleo hayana vyama!
 
Membe na Magufuli ndio itanoga......ili tuone kile ccm walichomwohopea Membe hadi kumfuta uanachama!
 
Kwann hutaki mwenyekigoda wa chama chakavu awepo bwashee?
 
Wamuongeze na jiwe na huo mdaharo uwe wa lugha ya kizungu[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kweli CCM madish yameyumba sasa upinzani kwa upinzani mdahalo wa nini?
 
..kunatakiwa mdahalo wa wagombea wote wa Uraisi ambao watapitishwa na NEC.

..mgombea ambaye naamini atafanya vizuri ktk mdahalo kuliko wenzake ni Prof.Nguyuru Ibrahim Haruna Lipumba.

..mgombea ambaye nadhani atafanya vibaya kuliko wote ni Dr.John Pombe Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…