Elections 2010 CHADEMA na kampeni kwa njia ya Mtandao

Mkuu mwiba, wewe pamoja na Lipumba, Duni, Hamad na Malaria Sugu wote mnakaribishwa viwanja vya Jangwani kama mpo Dar es Salaam, huenda mkapewa nafasi ya kuwasalimia wananchi.
Duh, punguza munkari Mkuu Mwiba na vuta subira, mwali atafunuliwa muda si kitambo. Baada ya ndoa ya mkeka ya CCM na CUF, hawa wamekuwa wamoja hakuna wa kuwatenganisha tena. Chadema kwa ufahamisho wako hawana kawaida ya kuwa na wagombea wa kudumu.
Hamna taabu hilo hata lisikupe homa, mwali kachumbiwa lakini kwa kuwa keshamchagua mume fisadi, kaonyesha ulipo uaminifu wake. Kadanganyika kwa kudhani yote yanayong'aa ni dhahabu lakini October 31 atabaki akilalama tu laiti angejua !
Ungekuwa mkweli ungejua wanaokuzwa na magazeti ni akina nani. Jaribu tu kufungua Daily Noise au Issa Supu blog au RadioTV ya Mafisadi utawaona bila wasi wasi.
Hawa akina Slaa Mbowe Zitto si walikuwemo humu jamii forum mbona wameingia mitini ? CUF wataongoza tena katika ushindi na wataendelea kuwa ni chama hiki tu kinachoweza kuwasiliza CCM na si vinginevyo.
Mkuu Mwiba jaribu kuwa na heshima kidogo unapowataja hao makamanda lakini uko sahihi kudai kuwa CUF ndio wanaweza kuwasiliza (sic!) CCM - si wana chanja kitanda ? Chadema hawana cha mseto, ebo !
Waulize Mpanda, Morogoro, Iringa, Mtwara, Kigoma, Mbeya, Mwanza, Kagera, Mara, Tabora...... bila kusahau Dar es Salaam. Haya Mkuu Mwiba, Chadema ni wababaishaji !
 
Nguvu ya internet sio ya kupuuzwa ndugu zangu, eti kwa sababu wanaotumia ni wachache. If that was a case, sasa hivi tunachat kwa sababu ya net. Hakukuwa na haja ya kufungua website kama tunadhani haiongezi value.. come on people....
Mkuu sidhani kama kuna mtu amekataa matumizi ya Mtandao isipokuwa uwezo wake kujitangaza ni mdogo sana ukilinganisha na mbinu nyinginezo.

Yes, tupo hapa mtandaoni na tunazungumza kila siku lakini ukweli umesimama wapi?.. Ni asilimia chini ya 1 ya Watanzania na hasa wapiga kura wanapitia JF tena naweza kusema ni hesabu hiyo kwa watu wanaoifahamu JF ni kitu gani..

Na jumlisha na blog zoote bado hatufiki asilimia na utakuta wnaaoingia mtandaoni kwa hiyo asilimia moja bado ni watu wanaoishi nje ya nchi. Ndio maana nikasema Chadema wanatakiwa kuzingatia sana WATU na MAZINGIRA yao ktk kila mbinu ya kujitangaza iwe sera ama Ilani na mengineyo.

Kama CCM wametumia sms haina maana Chadema au CUF wasitumie pia. CCM wanatumia sana magazeti, TV, redio na sms kwa sababu wanajua watawakamata wapi Watanzania wengi wapiga kura. Kinachotakiwa kwa chadema ni kufanya zaidi ya CCm sio kuogopa kutumia mbinu walizokwisha zitumia CCM.


Kuna mtindo mpya wa kunadi Bongo ambao unatumika sana hadi mikoani nao ni kukodosha lori la semi trailer lenye kuvuta behewa wazi kiwa unapigwa mziki huku MC akidondoa kulikoni..Nimeyaona mashirika mengi hasa ya simu wakitumia njia hii, inaudhi sana kwa watu mitaani kupigiwa ngoma na makelele lakini ndio inauza. Hivyo Chadema wanaweza kutumia kitu kama Mdundiko,Mchhiriku na kadhalika (Dar) au ngoma za kiasili (kikabila) huko mikoani ktk kila jimbo wakimnadi mgombea wao.

Mtandao pia utumike na hakika pamoja na kuwepo website ya Chadema sikumbuki lini mara ya mwisho nimepitia pale. Na hata hapa nilipo pamoja na kuwa majuu pia sikumbuki ni lipi nimewahi kupitia website ya chama chochote cha kisiasa iwe ni wakati wa uchaguzi au wakati wowote ule. Mara nyingi watu tunaingia ktk mtandao kutafuta vitu tunavyovipenda kuvisoma, burudani ya roho wakati umechoka na maisha (siasa) ili ujipumzishe na raia wengine.
 
huu ni uchumbuzi akinifu
 
Malaria Sugu tuambie hilo Gazeti la CCM (Uhuru) lilikuwa linasema nini hasa kuhusu Dkt Slaa kuwa na adabu, maana watu wameanza kuchangia hoja ambayo haieleweki!
 
kwa hiyo huo ndio msimamo rasmi wa chadema wa serikali tatu?

watu wa karatu na mikoa wengine wanaujua msimamo huu?
 

Mara nyingi Wazanzibar hawana 'impact' kubwa kwenye siasa za Tanzania. rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na rais wa Zanzibar wote wanachaguliwa na wabara.
 
Kwanza Slaa alienda kutafuta nini nchi jirani.
 
Kweli sasa naona watanzania wanafunguka akili au walikwisha funguka tu ila ni uoga,,

huyu lipumba badala ya kupigana kuitoa CCM yeye anahangaika na CHADEMA,,, huyu nahisi ni mamluki wao..... Yeye amshukuru Maalim Seif anambeba Zenji na mwenzie anapata cheo yeye ataishia kelele tuu!!

sisi tunataka mabadiliko makubwa hii nchi inatia aibu!!!
 
Usitake kuanzisha mengine kwani hujui zanzibar ni nchi.

Ninavyofahamu Katiba ya Zanzibar, 1984 inasema kwamba:

1. "Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!" (Ibara ya 1).
2. "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano akishauriana na Rais (wa Zanzibar) aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa." (Ibara ya 2 (2)).

Kwa hiyo Slaa akiingia Ikulu anaweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa na Wilaya, kwa hiyo lazima ajue maeneo ambayo atayagawa, akiona inafaa, kuanzia Novemba 1, 2010!
 
zenji nani hajui kuhusu udini ulivyowafunika???????????wangesikia cuf wameingia aaaaahhh hapo ndio penyewe kwani kuna waislamu tu na kama wakisikia jk mwislamu mwenzao kaenda aaahhh hapo fasta...UDINI...UDINI...UDINIII TATIZO ZENJI
 
Angeripoti mtu mwangine ningeamini hii hadithi.

Kumbe MS hata wewe unahudhuria mikutano ya Slaa!!!!!!?
 
Wazenji of coz hawana haki ya kuchagua sio raisi wa Tanzania tu, hata wa kwao. Kwani unadhani mwaka huu walimtaka Shein?
 
Sasa bendera tele ziliwekwa na nani? Au huko zenj bendera zatembea weye?
 
Nimeambiwa kwamba yule Profesa wa Pumba ameshachukua fomu kutoka NEC. Ni kweli jamani? Mbona kimya? Alichukua usiku? Nasema hivyo kwa sababu shamrashamra hazikuwepo! Natoa hoja hii kwa sababu CUF ni chama mbadala cha MS -- alitamka mwenyewe. Mwaka 2005 CUF iliambulia ZERO Wabunge huku Bara na safari hii itakuwa MINUS ZERO!!!! Twangojea kuizika CUF rasmi huku Bara ifikapo Novemba -- na hapo ndipo mtakapon'gamua faida ya kuingia ndoa na Chama cha Mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…